Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


WANAFAMILIA SITA WALIOTEKETEA KWA MOTO WAZIKWA JIJINI DAR


Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal akiweka shada la maua katika mojawapo ya makaburi ya wanafamilia.Mojawapo ya jeneza likishushwa kaburini.Ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati wa mazishi.Mmoja wa wanandugu akipewa huduma ya kwanza baada ya kuanguka wakati wa mazishi hayo.MAKAMU wa Rais, Dk. Gharib Bilal leo amewaongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam katika mazishi ya watu sita wa familia moja waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea wiki iliyopita huko Kipunguni...

Vijimambo

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mwananchi

Ni simanzi na vilio mazishi ya wanafamilia sita Dar

>Huzuni, simanzi na majonzi jana vilitawala maeneo ya Kipunguni A na baadaye kwenye Makaburi ya Airwing Ukonga, Ilala wakati miili ya watu sita waliofariki dunia kwa kuungua moto Jumamosi alfajiri ilipozikwa.

 

9 years ago

Vijimambo

HABARI KAMILI YA WATU 9 WALIOTEKETEA KWA MOTO BUGURUNI

WATU tisa wa familia moja wamekufa kwenye ajali ya moto ulioteketeza nyumba yao jijini Dar es Salaam, huku baba wa familia akinusurika kwa kuwa alikuwa amekwenda msikitini kuswali.

Nyumba hiyo iliyoteketea iko Mtaa wa Gulam katika eneo la Buguruni Malapa na baba wa familia hiyo, Masoud Matal hali yake ni mbaya. Marehemu hao walizikwa jana katika makaburi ya Kisutu.

Wakizungumza na mwandishi, majirani walisema marehemu hao walikutwa wamekumbatiana baada ya kupiga kelele kwa muda mrefu wakiomba...

 

10 years ago

Habarileo

JK atoa pole kwa ndugu walioteketea kwa moto

RAIS Jakaya Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki kuomboleza vifo vya watu sita wa familia moja waliopoteza maisha kwa ajali ya moto usiku wa kuamkia Jumamosi, Januari 7, 2015, katika eneo la Kipunguni A, Ukonga Banana, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

 

10 years ago

Vijimambo

WATU SITA WATEKETEA KWA MOTO KIPUNGUNI, DAR

Watu sita wameuawa kwa moto baada ya nyumba inayomilikiwa na mzee David Mpili, kuteketea kwa moto huko Kipunguni Ukonga jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumamosi Februari 7, 2015. Taarifa zinasema, familia hiyo ambayo ina uhusiano na waziri wa nchi ofisi ya rais kazi maalum, Profesa Mark Mwandosya iliokana na hitilafu ya umeme. profesa Mwandosya mwenyewe ni miongoni mwa wau waliofika kwenye eneo la tukio mapema leo hii Jumamosi, ili kuwapa pole na kujionea uharibifu na maafa...

 

10 years ago

GPL

MWILI WA AISHA MADINDA WAZIKWA MAKABURI YA KIBADA, KIGAMBONI JIJINI DAR

Maziko ya mwili wa marehemu Aisha Madinda yakifanyika katika makaburi ya Kibada, Kigamboni jioni hii. Mwili wa Aisha Madinda ukishushwa kaburini.…

 

10 years ago

CloudsFM

Makamu wa rais, Dk. Bilal ahudhuria mazishi ya ndugu sita waliokufa kwa ajali ya moto Dar.

MAKAMU wa Rais, Dk. Gharib Bilal leo amewaongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam katika mazishi ya watu sita wa familia moja waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea wiki iliyopita huko Kipunguni jijini Dar es Salaam.Mazishi hayo yamefanyika leo katika makaburi ya Airwing, Keko jijini Dar e s Salaam huku yakiuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama na serikali, taasisi na makampuni binafsi.Akizungumza kwa huzuni wakati akiwapa pole ndugu, majirani, marafiki...

 

10 years ago

Mwananchi

Familia yateketea kwa moto jijini Dar

 “Yesu tuokoe, Yesu tuokoe”. Ndiyo sauti ya mwisho iliyosikia toka kwenye nyumba ya vyumba vitatu na sebule iliyoteketea kwa moto na kusababisha watu sita wa familia moja kupoteza maisha, huku miili ya baba na mama wa familia hiyo ikikutwa pamoja imekumbatiana, ikiwa ni ishara ya kufa pamoja.

 

10 years ago

GPL

PIKIPIKI YATEKETEA KWA MOTO UBUNGO JIJINI DAR

Wananchi wakishuhudia pikipiki iliyoteketea kwa moto baada ya kugongana na daladala eneo la Ubungo Mataa mchana huu. Dalaldala aina ya DCM linalofanya safari zake kati ya Mbagala - Ubungo baada ya kugongana na pikipiki iliyoteketea.…

 

10 years ago

Habarileo

Abiria ajali ya moto wazikwa kaburi moja

Maziko ya mabaki ya miili ya abiria waliokuwa katika basi la Nganga lililoungua moto baada ya kugongana na Fuso mkoani Morogoro, yakifanyika katika kaburi la pamoja.MAELFU ya wakazi wa Tarafa ya Kidatu wilaya ya Kilombero na Mikumi, wilayani Kilosa mkoani Morogoro, walijawa na simanzi kubwa zilizotawaliwa na vilio wakati wa maziko ya miili ya watu 15 waliozikwa jana kwenye kaburi moja, ikiwa ni siku moja baada ya kufa kwa kuteketea kwa moto baada ya basi walilokuwa wakisafiria la Kampuni ya Nganga Express kulipuka lililopogongana na lori aina ya Mitsubishi Fuso.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani