Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


YADI YA MABOMBA YA GESI KONGOWE DAR YAFUNIKWA NA MAJI

Kutokana na hali hiyo magari yamefunikwa na maji, hivyo kusababisha kazi kusimama na wigo uliozungushiwa mabati kubomoka na 'mateja' kujitwalia mabati hayo, hivyo kuwa neema kwao. Wakati huo huo usafiri wa mabasi kutoka Mbagala kwenda Kongowe umesimama kutokana na magari mengi kuzimika katikakati ya barabara hiyo, hivyo hivi sasa kuna msururu wa watu wanaotembea kwa miguu kwenda Kongowe au kutoka Kongowe kwenda Mbagala. ...

GPL

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

DAR YAFUNIKWA NA MAJI KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA, WANANCHI WAKOSA MAKAZI


 Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.


MAFURIKO,Mafuriko,Mafuriko .! Jiji la Dar limejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha wengine kukosa makazi.


Maeneo yaliyokumbwa kwa mafuriko ni Mnyamani (Ilala),Bonde la Mpunga (Kinondoni) ,Kigogo (Kinondoni),Mikocheni ( Kinondoni),Vingunguti (Ilala) Tabata Kisiwani (Ilala)na Kurasini (Temeke) na maeneo mengine ambayo hayajawahi kupata mafuriko yamefika.


Mvua hizo zimeharibu miundombinu katika barabara ya Morogoro kwa kujaa...

 

11 years ago

Michuzi

shehena ya mwisho ya mabomba kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi yawasili dar

 Katibu mkuu wizaraya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (Watatu kushoto), akizungumza jambo na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa (Wanne kushoto), wakati kamati hiyo ilipotembelea bandari ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kujionea kazi ya upakuaji vifaa vya ujenzi na kupokea shehena ya mwisho ya mabomba ya kupitishia gesi. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, Raha Mohammed (Kulia), Richard Ndasa (Wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo...

 

11 years ago

Michuzi

KONGAMANO LA MAJI LAFANYIKA JIJINI DAR,WADAU WAJIONEA TEKNOLOJIA MPYA YA MABOMBA

Wiki hii jijini Dar es salaam kumefanyika Kongamano kubwa la wadau wa maji kutoka kila kona ya nchi hii. kubwa lililofanyiwa kazi na wataalam hao wa maji ni kujulishwa teknolojia mpya ya mabomba iliyokuwa inatambulishwa na kampuni kubwa ya teknolojia ya mambomba ya Borouge kutoka Falme za Kiarabu. 
Borouge ilileta wataalam wanne ambao ni Mario Andrade, Farraj Tashman, Andrew Wedgner na Reda Ashkar. walionufaika na mafunzo hayo ni waliotoka Mamlaka za Maji mijini na vijiji, Wahandisi,...

 

11 years ago

Michuzi

KONGAMANO LA MAJI LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM, WADAU WAJIONEA TEKNOLOJIA MPYA YA MABOMBA

WIKI HII JIJINI DAR ES SALAAM KUMEFANYIKA KONGAMANO KUBWA LA WADAU WA MAJI KUTOKA KILA KONA YA NCHI HII.  KUBWA LILILOFANYIWA KAZI NA WATAALAM HAO WA MAJI NI KUJULISHWA TEKNOLOJIA MPYA YA MABOMBA ILIYOKUWA INATAMBULISHWA NA KAMPUNI KUBWA YA TEKNOLOJIA YA MAMBOMBA YA BOROUGE KUTOKA FALME ZA KIARABU.  BOROUGE ILILETA WATAALAM WANNE AMBAO NI MARIO ANDRADE, FARRAJ TASHMAN, ANDREW WEDGNER AND REDA ASHKAR. WALIONUFAIKA NA MAFUNZO HAYO NI WALIOTOKA MAMLAKA ZA MAJI MIJINI NA VIJIJI, WAHANDISI,...

 

10 years ago

Mtanzania

Mtwara yafunikwa na maji

mafurikoNa Florence Sanawa, Mtwara
NYUMBA zaidi ya 200 zimezingirwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha hali iliyosababisha mafuriko makubwa na kuzua taharuki kwa wakazi wa maeneo ya Kiyangu B, Kisutu, Ligula na Mdenga.
Mvua hiyo iliyoanza kunyesha saa 8 usiku wa kuamkia jana hadi saa 11 alfajiri imeharibu makazi ya watu na miundombinu katika mji wa Mtwara.
Kutokana na hali hiyo iliulazimu uongozi wa mkoa kuitisha kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ambapo walijadili hali hiyo na kufanya ziara ya...

 

11 years ago

Michuzi

Rotary Club Dar es Salaam wazindua mabomba ya maji safi na salama ya kunywa katika Shule ya msingi ya Kijitonyama

Wawakilishi kutoka Rotary Club Dar es Salaam wakizindua mabomba ya maji safi na salama ya kunywa katika Shule ya msingi ya Kijitonyama kupitia mradi wa Rotary wa “Maji kwa Maisha”. Kutoka kushoto ni Rais wa klabu ya Rotary ya Mikocheni John Gitonga akiwa na Naibu Mwenyekiti wa Rotary Tanzania Sharmila Bhatt, mratibu wa Elimu kutoka manispaa ya Kinondoni Alexandrina Kahandoma na kulia ni Jane Pesha kutoka klabu Rotary ya Mikocheni. Mradi huo uligharimu kiasi cha Sh 15 milioni.

 

11 years ago

Habarileo

Shehena ya mwisho ya mabomba ya gesi yawasili

Eliakim Maswi SHEHENA ya mwisho ya mabomba ya gesi imewasili Dar es Salaam jana ikitokea China na kuleta uhakika wa kukamilika kwa wakati kwa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, ifikapo Juni mwaka huu.

 

11 years ago

Tanzania Daima

Kitwanga apokea shehena ya mwisho mabomba ya gesi

NAIBU Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia nishati, Charles Kitwanga, amepokea shehena ya mwisho ya mabomba ya gesi katika Bandari ya Mtwara na kueleza ujio wa miundombinu hiyo ni neema...

 

11 years ago

Michuzi

NAIBU WAZIRI CHARLES KITWANGA APOKEA SHEHENA YA MWISHO YA MABOMBA YA GESI

Na Asteria Muhozya, Mtwara   Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Mhe. Charles Kitwanga, amepokea Shehena ya mwisho ya mabomba ya gesi katika bandari ya Mtwara na kueleza kuwa, ujio wa miundo mbinu hiyo ni neema kwa uchumi wa Tanzania.  Aliongeza kuwa, hiyo ni hatua kubwa katika kufikia malengo tarajiwa ikizingatiwa kwamba, kukamilika kwa mradi huo kutachochea na kufungua njia mbalimbali za uchumi unaoendana na sekta ya gesi na mafuta.   “Ujenzi wa miundombinu ya...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani