Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Ajali ya Hiece yaua 12 Arusha

WATU 12 wamekufa papo hapo katika ajali iliyotokea jana wilayani Arumeru, Arusha ikihusisha basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace na lori la mafuta, aina ya Scania. Ingawa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo licha ya mara kadhaa kupigiwa simu yake ya kiganjani iliyoita bila ya kupokewa, mwandishi wa habari hizi alishuhudia miili ya watu hao ikipokewa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, majira ya saa 12 jioni.

habarileo

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

GPL

AJALI YAUA 7 JIJINI ARUSHA

Watu saba wamefariki dunia papohapo na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya malori mawili kugongana katika eneo la Mti Mmoja wilayani Monduli mkoani Arusha.

Related News:

HOOD LAUA WATANO ARUSHA

Watu 5 wamekufa baada ya basi la Hood kwenda Mbeya kugongana na Hiace eneo la Kilala, Arusha asubuhi hii, wengi wajeruhiwa. Taarifa zaidi baadaye. GPL SOMA ZAIDI

...

 

11 years ago

Mtanzania

Ajali yaua 19

Ajali ya basi la Morobest iliyotokea mkoani Dodoma

Ajali ya basi la Morobest iliyotokea mkoani Dodoma

Debora Sanja, Dodoma na Fadhili Athumani, Mwanga

WATU 19 wamepoteza maisha na wengine 64 wamejeruhiwa katika ajali mbili zilizotokea katika mikoa ya Dodoma na Kilimanjaro.

Habari kutoka mkoani Dodoma zinasema watu 17 wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori.

Ajali hiyo ilitokea jana saa 2 asubuhi, katika eneo la Pandambili, lililoko Barabara ya Dodoma-Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari...

 

10 years ago

Habarileo

Ajali yaua 23

Mkuu wa wilaya ya Mufindi, Mboni Mhita akiwatembelea majeruhi hospitali ya Wilaya mjini Mafinga (Picha na Frank Leonard).WATU 23 wamekufa katika ajali iliyohusisha basi na lori mjini Mafinga, Iringa huku wengine 34 hali zao zikiwa mbaya.

 

11 years ago

Tanzania Daima

Ajali yaua 21

WATU 21 wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Mkupuka, Kibiti, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani. Watu...

 

11 years ago

GPL

AJALI YAUA 30 MWANZA

WATU 30 wamepoteza maisha huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya basi la Luhuye walilokuwa wakisafiria kutoka Musoma kwenda Mwanza kugonga mti na kupinduka wilayani Busega leo saa 3 asubuhi!

 

10 years ago

GPL

AJALI YAUA 33 MISRI

 Eneo maarufu kwa mapumziko nchini Misri, Sharm El-Sheikh. WATU 33 wamefariki dunia huku 41 wakijeruhiwa baada ya mabasi mawili kugongana katika Peninsula ya Sinai, Misri asubuhi hii. Mabasi hayo yalikuwa yamebeba watu waliokuwa wakielekea katika mapumziko eneo la Sharm El-Sheikh lililopo kwenye Peninsula ya Sinai. Basi moja lilipinduka baada ya ajali hiyo ikiwa ni kilomita 50 kutoka eneo hilo la mapumziko. Mabasi hayo...

 

10 years ago

Habarileo

Ajali yaua 2 yajeruhi 45

David Misime.WATU wawili wamekufa papo hapo huku wengine 45 wakijeruhiwa baada ya basi la abiria lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso na roli katika kijiji cha Vikonje wilayani Chamwino mkoani hapa.

 

10 years ago

GPL

AJALI YAUA 35 MUSOMA

WATU zaidi ya 35 wamefariki dunia katika ajali mbaya iliyoyahusisha magari matatu, mawili mabasi ya abiria na moja gari dogo aina ya Nissan Terano leo asubuhi eneo la SabaSaba, mjini Musoma.
Ajali hiyo imetokea baada ya basi la Kampuni ya J4 Express lenye namba za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari mkoani Mara kuligonga ubavuni gari dogo aina ya Nissan Terano lenye namba za usajili T 332 AKK na kulitupa mtoni kisha kugongana uso kwa uso na basi lingine la Kampuni...

 

11 years ago

GPL

AJALI YAUA 8 NJOMBE

WATU nane wamefariki dunia huku wengine wakijeruhiwa baada ya lori lililobeba shehena ya mpunga lililokuwa likitokea Chimala mkoani Mbeya kuelekea Makambako mkoani Njombe kupata ajali na kutumbukia katika Mto Halali leo asubuhi wilayani Wanging'ombe, Njombe. Lori hilo lilitumbukia mtoni baada ya kugonga ukingo wa daraja la mto Halali. Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Esterina Kilasi amethibitisha kutokea tukio… ...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani