BANK OF AFRICA-TAZANIA, YAZINDUA UCHANGIAJI MATIBABU KWA WATOTO WALIOPINDA MIGUU
NA FRANCIS DANDE
BANK OF AFRICA-TANZANIA, leo imezindua rasmi kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia Hospitali ya CCBRT katika mpango wake wa kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kupinda miguu.
Msaada huu kwa Hospitali ya CCBRT utawezesha watoto kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kupata matibabu bure au kwa gharama nafuu ili kuwawezesha kutembea sawa sawa.
Ugonjwa wa kupinda miguu unaweza kuathiri mguu mmoja au yote miwili. Miguu iliyopinda...
Michuzi