Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Dar yapiga marufuku vyakula mitaani kudhibiti kipindupindu

SaidiMeckSadickNa Waandishi wetu, Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, amepiga marufuku uuzwaji wa vyakula na matunda katika maeneo yasiyorasmi.

Agizo hilo limelenga kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea kusambaa katika jiji la Dar es Salaam, ambapo hadi sasa watu watatu wameripotiwa kupoteza maisha.

Sadick alitoa amri hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kusema wagonjwa wa kipindupindu wamefikia 56.

“Wagonjwa...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

StarTV

Uuzwaji matunda, vyakula maeneo ya wazi ni marurufu nchini ili Kudhibiti Kipindupindu

Serikali imepiga marufuku wafanyabiashara wanaouza matunda yaliyokatwa na chakula katika maeneo ya wazi nchi nzima ili kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ulioenea katika mikoa takribani 21 Tanzania Bara.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa tamko hilo la serikali na kusema ili kuumaliza ugonjwa huo ni lazima maambukizi mapya yadhibitiwe na atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Tamko hilo limetolewa wakati watu elfu 11,257...

 

9 years ago

StarTV

Polisi Kanda maalum Dar yapiga marufuku maandano ya Chadema.  

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam limezuia  maandamano ya wananchama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yasiyo kuwa na kikomo  kwasababu ni kinyume na sheria.

Maandamano  ya wafuasi  wa CHADEMA yalipangwa kufanyika  kuanzia  Novemba 3 mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam  kudai uporwaji wa Demokrasia dhidi ya mgombea wao Edward Lowassa.

Ni kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Kamanda Suleimani Kova akitoa tamko la...

 

9 years ago

Raia Tanzania

Vyakula shuleni na kipindupindu

AGOSTI 18, 2015 Dar es Salaam ilipata taarifa mbaya ya mlipuko wa Kipindupindu, mtu mmoja aliugua na kufariki.

Ingawa baadaye ulisambaa hadi Morogoro, kwa sasa jijini hapa idadi inaongezeka siku hadi siku. Takwimu za mwishoni mwa mwezi uliopita zinaonyesha kuna wagonjwa 417.

Kwa mujibu wa maofisa afya, ugonjwa huu unasababishwa na uchafu hasa ulaji wa kinyesi kibichi bila kufahamu na hivyo kushauri jamii kuzingatia usafi hasa waendapo maliwatoni, wahakikishe wananawa kwa sabuni kila...

 

9 years ago

Habarileo

Moro wajipanga kudhibiti kipindupindu

MKUU wa mkoa wa Morogoro (RC), Dk Rajab Rutengwe, amewataka watendaji wa kata na mitaa katika halmashauri za mkoa huo kuhakikisha kila mmoja anawajibika ipasavyo kusimamia suala la usafi wa mazingira na kuzuia uuzaji holela wa vyakula na matunda.

 

10 years ago

Habarileo

Kigoma wafunga visima kudhibiti kipindupindu

 Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma, Leonard SubiWAKATI ikielezwa kuwa ugonjwa wa kipindupindu bado unaendelea kuwasumbua wakazi wa mkoa Kigoma, kwa kuendelea kuwepo kwa wagonjwa wapya serikali imeanza kuchukua hatua kukabiliana na hali hiyo, ikiwemo kuvifunga baadhi ya visima vilivyokuwa vikitumiwa na wananchi kwa maji ya majumbani.

 

9 years ago

Mwananchi

Juhudi zaidi zifanyike kudhibiti Kipindupindu

Hadi sasa, watu 36 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu. Idadi hiyo ni watu 33 zaidi ya waliofariki ulipolipuka Agosti 15, jijini Dar es Salaam na wengine 26 walilazwa katika hospitali za Mwananyamala na Sinza.

 

9 years ago

Habarileo

WHO yatoa dawa, fedha kudhibiti kipindupindu

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imepewa msaada wa vitu mbalimbali zikiwemo dawa zenye thamani ya Sh milioni 42.2 pamoja na fedha taslimu milioni 160 kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu.

 

9 years ago

Habarileo

Wazuiwa chakula holela kudhibiti kipindupindu

WAKAZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu wametahadharishwa kujikinga na kipindupindu, ugonjwa ulioingia kwa kasi wilayani humo kutoka wilaya jirani ya Kwimba mkoani Mwanza.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani