Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Hakimu kesi ya mauaji ya Dk. Mvungi ajitoa

mvungiNa Kulwa Mzee, Dar es Salaam
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Waliarwande Lema, amejitoa kusikiliza kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi, inayowakabili washtakiwa 11.
Tukio hilo lilitokea juzi, baada ya washtakiwa hao 11 kumuomba Hakimu Lema ajitoe kuisikiliza kesi yao ili iweze kupangwa kwa hakimu mwingine ambaye wao wanaona atawatendea haki.
Kutokana na ombi hilo, Hakimu Lema alijitoa na kuiahirisha kesi hiyo...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mwananchi

Hakimu ajitoa kesi ya jumuiya ya Uamsho

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Hellen Liwa amejitoa kusikiliza kesi ya ugaidi inayowakabili viongozi 23 wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI).

 

10 years ago

Habarileo

Hakimu ajitoa kesi ya ugaidi ya Shehe Farid

Shekhe Farid Hadi AhmedHAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Hellen Riwa amejitoa kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Shekhe Farid Hadi Ahmed na wenzake.

 

10 years ago

Vijimambo

Hakimu ajitoa kesi ya kina Sheikh Farid,

Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Ahmed
Hakimu Mkazi wa Mahakama Kisutu jijini Dar es Salaam, Hellen Riwa, amejitoa kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Ahmed na wenzake 21.

Hakimu Riwa amechukua hatua hiyo wakati upande wa washtakiwa ukiitaka mahakama imbadilishe kwa kutokuwa na imani naye.

Oktoba 1, mwaka huu, Hakimu Riwa alitoa...

 

11 years ago

Habarileo

Jaji Kaduri ajitoa kesi ya mauaji ya Profesa Jwani Mwaikusa

JAJI Lawrence Kaduri wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, amejitoa kusikiliza kesi ya mauaji ya watu watatu akiwemo aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sheria, Profesa Jwani Mwaikusa.

 

11 years ago

Habarileo

Jaji ajitoa kesi ya mfanyabiashara

JAJI Bethuel Mmila amejitoa katika jopo la majaji watano, wanaosikiliza rufaa ya mfanyabiashara Kibute Otienyeri, anayepinga adhabu ya kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kunajisi.

 

11 years ago

Habarileo

Upelelezi mauaji ya Dk Mvungi bado

UPELELEZI wa kesi ya mauaji ya Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Edmund Mvungi inayowakabili watu 10, haujakamilika.

 

10 years ago

Habarileo

Shahidi kesi ya rushwa ya Hakimu afariki dunia

UPANDE wa mashitaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), wameithibitishia Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwamba aliyetakiwa kuwa shahidi wa pili katika kesi ya rushwa ya Sh 50,000 inayomkabili Hakimu Grace Kivegele na Karani wake, Rose Kuhima wa Mahakama ya Mwanzo Buruguri, amefariki dunia.

 

10 years ago

Mwananchi

Kesi za madai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi

Mahakama ya Hakimu Mkazi imeanzishwa chini ya kifungu cha nne cha Sheria ya Mahakama Sura ya 11 kama ilivyorejewa mwaka 2002.

 

11 years ago

Habarileo

Hakimu achoshwa na Jamhuri kesi ya akina Mattaka

HAKIMU Mkazi Augustina Mmbando amesema upande wa Jamhuri unamkwaza kwa kitendo cha kuchelewesha kesi ya kulisababishia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) hasara ya Dola 143,442.75 za Marekani, inayomkabili Mkurugenzi mstaafu wa kampuni hiyo David Mattaka na wenzake.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani