Jaji amwonya wakili kesi ya Mwalle
NA JANETH MUSHI, ARUSHA
JAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Gadi Mjemas anayesikiliza kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Wakili Median Mwalle na wenzake watatu, amemwonya na kumtaka Wakili wa Jamhuri, Pius Hilla, amuulize shahidi wake kuhusu kesi iliyopo mahakamani na si kuuliza juu ya mafunzo.
Jaji Mjemas alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati akisikiliza ushahidi wa shahidi wa pili wa Jamhuri, Suleiman Nyakulinga, katika kesi inayoendelea kusikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania,...
Mtanzania
Habari Zinazoendana
9 years ago
Mtanzania22 Dec
Jamhuri yakata rufaa kesi ya Wakili Mwalle
NA JANETH MUSHI, ARUSHA
MAWAKILI wa Jamhuri katika kesi ya utakatishaji fedha haramu inayomkabili Wakili Median Mwalle na wenzake watatu, wamewasilisha kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania dhidi ya uamuzi wa Jaji Gadi Mjemas wa kukataa kuvipokea baadhi ya vielelezo vya ushahidi kutoka nchini Marekani.
Vielelezo hivyo viliwasilishwa mahakamni hapo na shahidi wa pili wa upande wa Jamhuri, Suleiman Nyakulinga wiki iliyopita.
Uamuzi huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Jaji Mjemas...
9 years ago
Mtanzania08 Dec
Jaji atupa hoja za utetezi kesi ya Mwalle
NA JANETH MUSHI, ARUSHA
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, imetupilia mbali pingamizi lililotolewa na mawakili wa utetezi katika kesi inayomkabili Wakili Median Mwalle na wenzake watatu.
Jaji Gadi Mjemas alitoa uamuzi huo jana aliposikiliza mashahidi wa pande zote mbili baada ya kutokea mvutano wa sheria ulioibua kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi kuhusiana na kupokelewa maelezo ya mshitakiwa wa nne, Elias Ndejembi.
Jaji Mjemas alisema baada ya kusikiliza pande zote mbili,...
10 years ago
Mtanzania03 Mar
Jaji Msengi Kusikiliza kesi ya Wakili Mwale
Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam
KESI ya utakatishaji fedha haramu inayomkabili wakili maarufu jijini Arusha, Medium Mwale na wenzake watatu, imeanza kusikilizwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mbele ya Jaji Fatuma Masengi.
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mwishoni mwa wiki baada ya Jamhuri kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Oswald Tibabyekomya, kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali ya mashtaka 42 yanayowakabili.
Tibabyekomya alidai washtakiwa wote walikubali majina yao kuwa Median Mwale, Don...
10 years ago
BBCSwahili09 Apr
Jaji na wakili wapigwa risasi Italy
9 years ago
Habarileo14 Dec
Jaji amtaka Wakili asipoteze muda
JAJI wa Mahakama Kuu, Jaji Gadi Mjemas anayesikiliza kesi ya kughushi nyaraka na kutakatisha fedha inayomkabili Wakili maarufu Median Mwale na wenzake watatu, amemtaka Wakili wa Serikali, Pius Hilla kumwelekeza shahidi wa kesi hiyo kitu gani alichunguza badala ya kumuuliza kozi alizohudhuria kwani zinapoteza muda.
11 years ago
Habarileo30 Apr
Wakili: Kesi ya Mwale ilifunguliwa kimakosa
UPANDE wa utetezi kwenye kesi ya wakili maarufu jijini hapa, Median Mwale na wenzake watatu ya kutakatisha fedha haramu, umedai mashitaka hayo dhidi ya washitakiwa, yalifunguliwa kimakosa kabla ya sheria iliyowashitaki kutungwa.
10 years ago
Mtanzania13 Sep
Wakili wa Mbasha augua, kesi yaahirishwa
![Emmanuel Mbasha](http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/07/Emmanuel-Mbasha.jpg)
Emmanuel Mbasha
Veronica Romwald na Zainabu Abdillah (MUM), Dar es Salaam
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala jana imeahirisha kesi ya ubakaji inayomkabili mfanyabiashara na muimbaji wa muziki wa injili, Emmanuel Mbasha hadi Septemba 19, mwaka huu kutokana na wakili anayemtetea, Mathew Kakamba, kuugua shinikizo la damu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwendesha Mashitaka wa Polisi na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai Mahakama ilifikia uamuzi huo baada ya Kakamba kuieleza Mahakama kuwa...
11 years ago
Tanzania Daima01 Aug
Kesi ya wakili Yasinta yapigwa kalenda
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni imeiahirisha kesi inayomkabili Wakili wa Serikali,Yasinta Rwechungura (44), Mkazi wa Boko Njiapanda, jijini Dar es Salaam hadi Agosti 29, mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika....
11 years ago
BBCSwahili08 Aug
Wakili wa Pistiorius asema kesi imevurugwa