Kortini kwa kulawiti mtoto
Maneno Selanyika na Ramadhani Mwakikato, Dar es Salaam
MKAZI wa Mbezi Beach Dar es Salaam, Tuntutye Mwasyete (25), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kumlawiti mtoto (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa mwaka mmoja.
Mbele ya Hakimu, Lilian Rutehangwa, Wakili wa Serikali Masini Musa alidai kwamba tukio hilo lilitokea Mei 14 mwaka huu huko Kawe.
Mtuhumiwa alikana shtaka hilo na alirejeshwa mahabusu hadi Juni 24 mwaka huu yatakaposomwa maelezo ya awali.
Mtanzania
Habari Zinazoendana
9 years ago
Mwananchi28 Nov
Kigogo CCM kortini kwa kulawiti wanawe
9 years ago
Mwananchi24 Dec
Jela maisha kwa kulawiti mtoto
10 years ago
Habarileo16 Nov
Padri aliyekuwa akitafutwa kwa kulawiti mtoto afariki
MTUHUMIWA wa kesi ya kulawiti mtoto wa kiume, aliyekuwa akitafutwa na Mahakama ya Rufaa, Sixtus Kimaro, ambaye alikutwa na tuhuma hizo wakati akiwa Padri katika Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, amefia nchini Msumbiji na mwili wake umesafirishwa kuja Dar es Salaam.
9 years ago
Mtanzania30 Dec
Polisi jela maisha kwa kubaka, kulawiti mtoto
Na Faraja Masinde, Dar es Salaam
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, imemhukumu askari polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, G 9762 PC Daniel (24) kutumikia kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na makosa ya kubaka na kumlawiti mtoto wa miaka 13.
Mbali na kifungo hicho, mtuhumiwa huyo ameamriwa kulipa fidia ya Sh milioni 2 ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Said Mkasiwa baada ya...
11 years ago
Mwananchi13 Feb
Kortini kwa tuhuma za kumshambulia mtoto
10 years ago
Habarileo09 Feb
Kortini kwa kumlawiti mtoto wake
MKAZI wa mtaa wa Migongo kata ya Migongo Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara, Hajili Mpili (52) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Masasi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.
10 years ago
Habarileo25 Sep
Mbaroni akituhumiwa kulawiti mtoto
POLISI mkoani Kagera inamshikilia mkazi wa Manispaa ya Bukoba, Jovin Kasuno (22) kwa tuhuma za kulawiti mtoto mwenye umri wa miaka sita na kumuumiza.
10 years ago
Habarileo14 Aug
Atuhumiwa kulawiti mtoto wa mkewe
MKAZI wa eneo la Majengo mjini Manyoni, Juma Saidi (32) anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kumlawiti mtoto wa mkewe. Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 14, anasoma Kidato cha Kwanza katika shule moja ya sekondari wilayani Manyoni na inadaiwa alifanyiwa kitendo hicho juzi saa 6 usiku nyumbani kwao.
11 years ago
Habarileo16 Feb
Kortini kwa kuua mtoto wakipigana na mama
MKAZI wa kijiji cha Mkangala katika Mji wa Namanyere Mkoa wa Rukwa, Charles Mtonja (19) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu wa Wilaya ya Nkasi akituhumiwa kumuua mtoto wake wa kike, Kolo Mtonja , mwenye umri wa mwaka mmoja kwa kumpiga na fimbo kichwani wakati akigombana na mama yake .