Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Kubenea apandishwa Mahakamani leo

said1Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.

Baada ya taflani iliyotokea jana Jumatatu kati ya mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea wa Chadema na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda eneo la viwanda (EPZA) Mabibo jijini Dar hali iliyopelekea DC Makonda kuwaamuru polisi wamuweke chini ya ulinzi Saed Kubenea na kumpeleka Kituo cha Polisi. Leo Saed Kubenea amepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa wilaya ya...

Global Publishers

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

StarTV

Mbunge Saed Kubenea apandishwa kizimbani

Mbunge wa Jimbo la Ubungo Saed Kubenea jana amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupandishwa kizimbani akikabiliwa na shitaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili Mkuu wa Serikali Timon Vitalis mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba amedai kuwa Desemba 14, 2015 katika kiwanda cha Tooku Garments Company Limited kilichopo Mabibo External Kebenea alitoa lugha chafu dhidi ya  Makonda.

 Wakili wa serikali Timon...

 

10 years ago

Mwananchi

AG, Kubenea sasa waitwa mahakamani

Hatimaye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana imetoa hati ya wito kwa pande zote, mlalamikaji na mlalamikiwa katika kesi ya mamlaka ya Bunge la Katiba ikiwataka kufika mahakamani.

 

10 years ago

Michuzi

Naibu Mwanasheria Mkuu amewasilisha Mahakamani pingamizi la awali dhidi ya kesi ya kuhoji mamlaka ya Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari Said Kubenea

Na Mwene Said wa Blog ya Jamii
NAIBU Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, leo amewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya kuhoji mamlaka ya  Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma iliyofunguliwa na  Mwandishi wa Habari Said Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwamba maombi hayo ni batili kisheria na hayawezi kuthibitishwa mahakamani, hivyo yatupiliwe mbali.
Masaju amewasilisha pingamizi hilo akitoa sababu nne, akiitaka mahakama kutupilia mbali maombi yaliyopo...

 

10 years ago

Michuzi

PROF. LIPUMBA APANDISHWA KIZIMBANI LEO

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Haruna Lipumba (katikati) akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo,alipofikishwa kujibu shitaka la kuhamasisha wanachama wa chama chake kufanya maandamano. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Haruna Lipumba akiwatuliza wanachama na wafuasi wa chama hicho kuacha kelele katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.Wanachama na Wafuasi wa CUF wakiimba nje ya Mahakama ya Hakimu...

 

10 years ago

Bongo Movies

Wema Sepetu Afunguliwa Apandishwa Kizimbani Leo!!

Mwigizaji wa filamu za kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ anapandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar kujibu kesi ya kushambuliwa vijana wawili, Rashid Balazi na Juma Bushiri, wakazi wa jijini Dar, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.

Katika kujibu kesi hiyo, Madam Wema hatakuwa peke yake kwani mpambe wake, Petit Man naye anahusika katika kesi hiyo kwa kuwa ndiye mshtakiwa wa kwanza.

Hivi karibuni kabla Madam Wema hajasafiri kwenda nchini Ghana kufanya...

 

9 years ago

Michuzi

MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO, SAID KUBENEA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO.

 Mbunge wa jimbo Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea amefikishwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam mapema hii leo akielekea katika  chumba cha kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. Mbunge wa jimbo Ubungo,(Chadema) Said Kubenea akiwa na wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo, leo mara baada ya kusomewa shitaka lililokuwa likimkabiri katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.  Mbunge wa jimbo Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea...

 

10 years ago

Michuzi

mtuhumiwa wa mauaji nchini uingereza apandishwa kizimbani mahakama ya kisutu jijini Dar es salaam leo


Mtanzania mwenye asili ya Kiarabu, Sammy al Mahri, aishiye Uingereza akiwa chini ya ulinzi wa polisi, wakati akipelekwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam,leo, kusomewa mashitaka ya kumuua mpenzi wake nchini Uingereza. Mahri anadaiwa kukimbilia Tanzania baada ya kufanya mauaji hayo. Picha na Khamis Mussa

 

10 years ago

Michuzi

CHID BENZ APANDISHWA KIZIMBANI JIJINI DAR LEO KWA SHITAKA LA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA,AKOSA DHAMANA, KESI YAKE KUTAJWA TENA NOVEMBA 11

MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi Abdallah Makwaro (29), maarufa kama Chid Benz, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.
Chid Benz amefikishwa  mapema leo saa 3:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusomewa mashitaka yake. Saa 7:50 mchana alifikishwa mbele ya...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani