Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Kumbukumbu ya Marehemu Saidaty Mfilinge

Miaka minne iliyopita, tarehe kama ya leo, ni siku ambayo hatuwezi kuisahau kamwe. Ni siku ambayo ulituacha ndugu zako katika majonzi makubwa sana. Ingawa hatukuoni, hatuongei na wewe, hatubadilishani mawazo kama ilivyokuwa wakati wa uhai wako, hatujaacha kukukumbuka na kukuombea kwa Mwenye ezi Mungu kila siku. Unakumbukwa sana Mama yako, ndugu na jamaa zako wote. Mwenye ezi Mungu Ailaze roho yako Mahala Pema Peponi, Amina. Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un!

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU BAKARI .M. NYAMBI

Familia ya Bw.BAKARI NYAMBI wa Temeke Dar es Salam wanakumbuka kifo cha baba yao mpendwa Bw.BAKARI NYAMBI kilichotokea tarehe 22.09.2014 siku ya Alhamisi na kuzikwa Ijumaa hapa DSM.Leo ni siku ya kumbukumbu yake mpendwa wetu Bakari Nyambi,kama ndugu jamaa na marafiki wa familia hiyo tunaomba kushirikiana katika kumuombea kwa mungu siku zote za maisha yetu.
Tulimpenda sana hila Mungu alimpenda zaidi (‘TUKUMBUKE MANENO WANAYOTUELEZA WAZAZI KWANI YANA FAIDA KWA MAISHA YA BAADAE HASA...

 

11 years ago

Michuzi

Kumbukumbu ya marehemu Lucy F. Njeama

Mpendwa wetu LUCY FIDELIS NJEAMA, Leo yapata miaka mitatu tangu siku ulipotutoka,lakini yaonekana kama ni Jana tu kwa jinsi ulivyotushiba. Unakumbukwa sana na mume wako, wanao Glory, Glady na Gallya, wazazi wako,dada na kaka zako na ndugu na Jamaa wote waliokupenda. Daima utabakia mioyoni mwetu tukikukumbuka kwa sala na maombi. Twamuomba Mungu akupokee katika ufalme wake, AMEN.

 

10 years ago

Michuzi

KUMBUKUMBU YA Marehemu ULLY HARUN KIWANGA

Bi. Pilly Mpenda na Familia ya watoto wa  marehemu Harun Kiwanga wanapenda kuwakaribisha katika Dua ya kumrehemu mpendwa wao ,Marehemu ULLY HARUN KIWANGA ambaye anatimiza mwaka mmoja toka kufariki kwake,hapo kesho siku ya Jumapili tarehe 15.3.2015 kuanzia saa 5 asubuhi nyumbani kwao Kinondoni Block 41. Karibuni sana

 

10 years ago

Michuzi

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MWALIMU NOVATI SIMEON RUTAGERUKA


TAREHE 5 - MEI - 2015, UMETIMIZA MIAKA MITANO TANGU MWENYEZI MUNGU ALIPOKUTWAA TOKA HAPA DUNIANI.  PAMOJA NA KWAMBA KIMWILI HAUPO NASI, KIROHO TUNAKUKUMBUKA DAIMA.
UNAKUMBUKWA DAIMA NA WATOTO WAKO FLORIDA, ILLUMINATA, LIBERATA, DUNSTAN, JOYCE NA EDWIN PAMOJA NA WAKWE, WAJUKUU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.


IBADA YA MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MWALIMU RUTAGERUKA ITAADHIMISHWA SIKU YA JUMANNE TAREHE  5 - MEI - 2015, KATIKA KANISA LA MTAKATIFU JOSEPH, DAR-ES-SALAAM, SAA 11.30 JIONI.


BWANA ALITOA,...

 

10 years ago

Vijimambo

Misa ya kumbukumbu ya Marehemu Michael Ndaskoi Mlingi .

Familia ya Geraldine Ngowi na Grace Mlingi wa Silver Spring, MD inapenda kuwashukuru wote kwa kushiriki kwa njia moja au nyingine kwenye misa ya kumbukumbu ya maisha ya Michael Ndaskoi Mlingi .Michael Mlingi alikuwa baba mzazi wa Grace Mlingi na tulimpoteza mwezi wa machi mwaka huu.misa hiyo ilifanyika Jumamosi May 16th 2015 katika kanisa la Saint Edward Roman Catholic Church 901 Poplar Grove St, Baltimore, Maryland 21216



ibada ikiendelea
Ndugu Kenneth Mshiu (binamu wa marehemu) akisoma...

 

11 years ago

Dewji Blog

Kumbukumbu ya miaka 6 ya marehemu Anthony Saimon Njeje

unnamed

Marehemu Anthony Simon Njeje Enzi za uhai wake.

Ni miaka Sita sasa imepita tangu ulipo enda kwenye makao ya kudumu.Hatupo nawe kimwili lakini kiroho upo nasi daima. Tunakukumbuka sana Baba yetu Mpendwa. Unakumbukwa sana na Mke wako Mpendwa Mama Elizabeth Anthony Njeje, Wanao Aninziye, Luseshelo-Ernest, Fredy na Sarah. Wajukuu zako Anthony Jr, Shikunzi-Alvin, Amarisa na Yasinta, Pia unakumbukwa na wafanyakazi wenzako wote wa Benki, majirani zako, waumini wenzako, ndugu Jamaa na Marafiki....

 

11 years ago

Dewji Blog

Kumbukumbu ya Marehemu Joachim Bwanampini Lebabu Kirambata

picha ya Marehemu Baba

KUZALIWA     02/02/1945          KUFA 04/05/2013

TAREHE 04/05/2014 UMETIMIA MWAKA MMOJA KAMILI TANGU

MWENYEZI MUNGU AKUITE.

ILIKUWA SIKU YA MAJONZI MAKUU KATIKA FAMILIA YETU.

KIFO KILITOKEA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI DSM.

UNAKUMBUKWA SANA NA  FAMILIA YAKO, MKE WAKO BI MARY KIRAMBATA, WATOTO WAKO LILIAN, JOSEPH, FILBERT, FLORENSO, FLORA, JANUARY, OCTAVIAN WAKWE ZAKO ENGELBERT, VIRGINIA, & DEVOTHA WAJUKUU ZAKO CELINE, MARYANNE, MELISA, ROSE, HENRICK, FLORENCE & JEREMIA NDUGU JAMAA...

 

9 years ago

Michuzi

IBADA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU GODFREY MNGODO, COLUMBUS, OHIO

Pr. Mwakabonga akiongoza ibada ya kumbukumbu ya marehemu Godfrey Mbiu Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini Marekani na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wafanyakazi wa kituo cha utangazaji Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili (VOA). Marehemu Godfrey Mbiu Mngodo aliaga Dunia Tarehe 11 Septemba, 2015 Dar es Salaam na kuzikwa Tanga. Godfrey Mbiu Mngodo amefanya kazi katika sehemu mbalimbali kama Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Voice of...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani