Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Ludewa kwa zidi kunoga,mkataba wa mamilioni wasainiwa kufikisha umeme mwambao wa ziwa Nyasa


Na Amiri kilagalila,Njombe

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umesainiana mkataba wenye thamani ya zaidi ya mil 920 na kampuni ya JV Mufindi Power Services Ltd wa kusabambaza umeme katika vijiji 4 vya tarafa ya mwambao wa ziwa Nyasa wilayani Ludewa mkoani Njombe ambavyo vimekuwa na changamoto hiyo kabla na baada ya uhuru .

Akizungumza mara baada ya kupokea  mkataba huo,mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrew Tsere amesema serikali imedhamilia kufikisha nishati ya umeme katika vijiji vyote wilayani...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

5 years ago

CCM Blog

MKATABA WASAINIWA KUFIKISHA UMEME MWAMBAO WA ZIWA NYASA, LUDEWA


Na Amiri kilagalila,Njombe 
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umesainiana mkataba wenye thamani ya zaidi ya mil 920 na kampuni ya JV Mufindi Power Services Ltd wa kusabambaza umeme katika vijiji 4 vya tarafa ya mwambao wa ziwa Nyasa wilayani Ludewa mkoani Njombe ambavyo vimekuwa na changamoto hiyo kabla na baada ya uhuru .
Akizungumza mara baada ya kupokea  mkataba huo,mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrew Tsere amesema serikali imedhamilia kufikisha nishati ya umeme katika vijiji vyote wilayani humo...

 

10 years ago

Habarileo

Mkataba wasainiwa mabasi ya kasi kuanza

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa GhasiaMIEZI imeanza kuhesabika kabla ya huduma ya usafiri kupitia mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam kuanza, baada ya mkataba kusainiwa kati ya serikali na wamiliki wa daladala kwa ajili ya kuendesha katika kipindi cha mpito.

 

11 years ago

Michuzi

MGOGORO WA ZIWA NYASA: WAKATI WENZETU MALAWI WAKIPAMBANA KWA TEKNOHAMA SISI WATANZANIA BADO TUNAPAMBANA KWA MANENO.

Kaka michuzi naomba unichapishie makala yangu kwenye blog yako. Kama tunavyofahamu kwa wakati huu Tanzania ipo katika mgogoro wa ziwa nyasa kati yetu na Malawi wenzetu wameenda mbali zaidi kwa kutumia mtandao wa Google Map.
Google Map ni mtandao mkubwa ambo unaonyesha Ramani ya dunia nzima kwa kutumia picha ya satellite na watu wengi hususani watalii hutumia mtandao huu kabla ya kwenda mahali husika . Lakini mtandao huu huitaji watu kujaza taarifa zaidi kama kuonyesha mipaka ya...

 

10 years ago

Michuzi

WANANCHI WA UKANDA WA ZIWA NYASA KUNUFAIKA NA UPATIKANAJI WA TAARIFA MAALUM ZA HALI YA HEWA KWA WAVUVI, WAKULIMA, WAFUGAJI NA WASAFIRISHAJI KWA WAKATI.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bi. Theo Ntara  ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela (watatu kutoka kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt. Hamza Kabelwa (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha inayohusu uboreshaji wa huduma za hali ya hewa katika maeneo ya Ziwa Nyasa kwa sekta ya wakulima na wafugaji, wavuvi na wasafirishaji, tarehe 14 Mei 2015  katika hotel ya Kyela Resort-Mbeya.Kwa chanzo na habari kamili BOFYA HAPA

 

10 years ago

StarTV

Magati yaanza kujengwa mwambao wa Ziwa Viktoria.

Na Maliganya Charahani,

Mwanza.

Mamlaka ya bandari nchini TPA imeanza kuziimarisha bandari zake katika mwambao wa Ziwa Viktoria kwa kujenga magati imara kwa ajili ya kuegeshea meli ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo na katika visiwa.

 

Uimara wa magati hayo utavutia pia kampuni ya huduma za meli kurejesha safari za meli kwenye maeneo hayo ambazo zilisitishwa kwa muda mrefu kutokana na miundombinu dhaifu.

 

Wakazi wa visiwani na mwambao wa Ziwa Viktoria wanatumia mitumbwi...

 

11 years ago

Habarileo

Utetezi wa Ziwa Nyasa

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ameweka wazi utetezi wa Tanzania katika mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na Malawi. Akizungumza na wahariri wa habari katika semina ya ardhi Dar es Salaam jana, Profesa Tibaijuka alisema tayari Rais Jakaya Kikwete ametoa ushahidi wa mpaka huo katika Kamati ya Marais Wastaafu, Festus Mogae wa Botswana, Joachim Chisano wa Msumbiji na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini.

 

10 years ago

Michuzi

MAFUNZO KWA WACHIMBAJI WA MADINI KUHUSU MATUMIZI YA HUDUMA ZA LESENI ZA MADINI KWA NJIA YA MTANDAO — KANDA YA ZIWA NYASA- SONGEA (7/8/2015) NA TUNDURU (9/8/2015)

Wizara ya Nishati na Madini inaendelea na mpango wake wa Mafunzo kwa Wachimbaji Madini Nchini kuhusu matumizi ya Mfumo wa Huduma za Leseni kwa njia ya Mtandao yaani Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP). Pamoja na malengo mengine, Mfumo huo umeanzishwa ili kutekeleza agizo la Serikali la kutaka Wizara na taasisi za Serikali ziwe zinapokea malipo ya Serikali kwa njia za kielektroniki. Mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa kwa wachimbaji wadogo nchi nzima ili kuwajengea uwezo.

 

10 years ago

Mtanzania

Filikunjombe: Ziwa Nyasa lipo salama

Deo-FilikunjombeNa Mwandishi Wetu, Ludewa
MBUNGE wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), amewataka wananchi wanaoishi mwambao wa Ziwa Nyasa kufanya shughuli zao, kwani mazungumzo ya kutafuta amani kati ya Tanzania na Malawi yanakwenda vizuri.
Kauli ya mbunge huyo imekuja huku nchi hizo zikiwa zimefikishana mbele ya jopo la viongozi wastaafu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), chini ya mwenyekiti wake Rais Mstaafu wa Msumbuji, Joachim Chisano.
Hayo aliyasema juzi katika mkutano wa hadhara...

 

10 years ago

Mtanzania

Malawi: Hakuna mjadala Ziwa Nyasa

Rais wa Malawi, Profesa Peter Mutharika

Rais wa Malawi, Profesa Peter Mutharika

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Malawi, Profesa Peter Mutharika, kwa mara nyingine amesisitiza kuwa Ziwa Nyasa linamilikiwa na nchi yake.

Kutokana na hali hiyo, amesema katu uongozi wake hautarajii kukaa katika meza ya majadiliano na nchi jirani ya Tanzania kuzungumzia umiliki huo.

Mutharika alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juzi mjini Lilongwe kuhusu ziara yake ya hivi karibuni jijini Washington DC, Marekani ambako alikuwa akishiriki...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani