Magufuli amkabidhi Nape wanamichezo, wasanii
RAIS John Magufuli amemteua Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo. Wakati wa kampeni zake za urais, Rais Magufuli mara kadhaa alikaririwa akisema atakuwa mstari wa mbele kuwasaidia wanamichezo na wasanii katika masuala mbalimbali wakati wa utawala wake.
habarileo
Habari Zinazoendana
9 years ago
Bongo517 Dec
Waziri Nape Nnauye afafanua jinsi wasanii chipukizi watakavyonufaika na sheria ya Radio na TV kuwalipa wasanii
![Katibu Mwenezi wa Itikadi wa CCM Nape NNauye akifuatilia mchezo kwa umakini mkubwa](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/07/Katibu-Mwenezi-wa-Itikadi-wa-CCM-Nape-NNauye-akifuatilia-mchezo-kwa-umakini-mkubwa2-200x134.jpg)
Kumeibuka maswali mengi toka ilipotangazwa sheria ya wanamuziki wa Tanzania kulipwa na vituo vya Radio na TV kwa kutumia kazi zao, moja wapo ni kuhusu kama sheria hii itakuwa na manufaa kwa wasanii wachanga au itachangia kuwapa wakati mgumu zaidi wa kupata nafasi ya kazi zao kuchezwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye amefafanua jinsi wasanii chipuziki watakavyonufaika na utaratibu huo unaotarajiwa kuanza kutumika mwezi January,2016.
“Wapo watu wanasema kwamba...
9 years ago
Mwananchi07 Nov
Wanamichezo wamwangukia Magufuli
9 years ago
Habarileo01 Nov
TASWA yampongeza Magufuli, wanamichezo
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), kimempongeza Dk John Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Tanzania. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto ilieleza kuwa chama hicho kina imani kubwa na Dk Magufuli na kumuahidi ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake.
9 years ago
Habarileo15 Dec
Nape aahidi raha wasanii
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema atahakikisha wanaimarisha eneo la sanaa ili liweze kufanikiwa na kuwa eneo linalojitegemea na linalojiimarisha vizuri na matunda yake kuonekana.
9 years ago
Bongo530 Dec
Redio na TV zitawalipa wasanii, asilimia 60 ya muziki utaochezwa lazima uwe wa nyumbani – Nape
![Waziri Nape akihojiwa](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2015/12/Waziri-Nape-akihojiwa-300x194.jpg)
Wakati baadhi ya wasanii na wadau mbalimbali wa burudani nchini wakiendelea kuwa na hofu juu ya mfumo mpya unaovitaka vituo vya redio na runinga kuwalipa wasanii mirahaba inayotokana na kucheza kazi zao, serikali imesema imeunda sheria ambayo itavifanya vishindwe kuepuka kucheza nyimbo za wasanii wa ndani.
Akizungumza na Bongo5 Jumanne hii kwenye uzinduzi wa filamu ya ‘Home Coming’ Mlimani City jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye alisema...
9 years ago
StarTV17 Dec
Nape aonya vyombo vya habari kutumia miziki ya wasanii bila idhini ya COSOTA
Serikali imetoa tamko kwa vyombo vyote vya habari nchini kuanzia january mosi mwakani kutokutumia miziki ya aina yeyote ule wa ndani au nje bila kibali kutoka Cosota.
Wakitoa tamko hilo kwa pamoja waziri wa habari michezo na utamaduni Nape Nnauye na waziri wa viwanda na biashara Charles Mwijage wamewataka wamiliki wa vyombo vya habari kutoa ushirikiano.
Nape amesema atalisimamia zoezi hilo na kutoa tahadhari kwa chombo chochote cha habari kitachokiuka tamko hilo hatakionea haya kukifungia...
9 years ago
StarTV17 Dec
Nape aonya vyombo vya habari kutumia muziki ya wasanii bila idhini ya COSOTA
Serikali imetoa tamko kwa vyombo vyote vya habari nchini kuanzia january mosi mwakani kutokutumia muziki wa aina yeyote ule wa ndani au nje bila kibali kutoka Cosota.
Wakitoa tamko hilo kwa pamoja waziri wa habari michezo na utamaduni Nape Nnauye na waziri wa viwanda na biashara Charles Mwijage wamewataka wamiliki wa vyombo vya habari kutoa ushirikiano.
Nape amesema atalisimamia zoezi hilo na kutoa tahadhari kwa chombo chochote cha habari kitachokiuka tamko hilo hatakionea haya kukifungia...
9 years ago
Habarileo27 Dec
Nape aomba Watanzania kumuombea Magufuli
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewaomba Watanzania kuendelea kumuombea Rais John Magufuli, kwani kazi ya kutumbua majipu ambayo ameianza ni kazi ngumu na yenye vikwazo.
9 years ago
Mtanzania11 Dec
Magufuli amteua Nape Wizara ya Michezo
NA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM
RAIS wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, ametangaza Baraza la Mawaziri na kumteua Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.
Awali kabla ya uteuzi wa jana wa Serikali ya Awamu ya Tano, wizara hiyo ilikuwa chini ya mbunge wa kuteuliwa Dk. Fenella Mukangara na Naibu Waziri wake Juma Nkamia ambaye ni Mbunge wa Chemba.
Akitangaza baraza hilo jana jijini Dar es Salaam, Rais...