Mbatia akosoa agizo ujenzi maabara
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia amesema agizo la ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari nchini,halikufuata taratibu na ndiyo sababu Serikali kuu na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) wanarushiana mpira juu ya agizo hilo.
Mwananchi
Habari Zinazoendana
10 years ago
Habarileo02 Dec
Dar yatekeleza agizo la maabara za JK
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akisubiria kupatiwa majibu juu ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari, kwa mujibu wa agizo lake kwa kila halmashauri za wilaya na manispaa nchini, manispaa za Dar es Salaam zimebainisha kuwa zinaendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa agizo hilo.
10 years ago
Habarileo04 Dec
Mlele waringia kutimiza agizo la maabara
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akisubiri kupatiwa majibu juu ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za kata nchini, Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imebainisha kutekeleza agizo hilo kwa kiwango cha juu.
10 years ago
Dewji Blog04 Nov
Agizo la kukabidhi vyumba vya maabara kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida bado kutekelezwa
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari kata ya Ikungi wilayani Ikungi mkoa wa Singida,wakishiriki ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara jana kama walivyokutwa na mpiga picha wetu. Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone, aliagiza akabidhiwe vyumba vitatu vya maabara kwa kila shule ya sekondari 153 za kata za mkoa huo kabla ya oktoba 15 mwaka huu.Mambo yamekuwa tofauti kwa shule ya sekondari ya kata ya Ikungi ambayo hadi sasa bado ujenzi upo ngazi ya msingi.(Picha na Nathaniel Limu).
10 years ago
MichuziUJENZI WA MAABARA: MAHIZA AWATAKA WAKUU WA IDARA WASIKAE OFISINI WAENDE KWENYE KATA,ATAKA MADIWANI WAAHIRISHE VIKAO VYAO HADI UJENZI UTAKAPOKAMILIKA
SUALA la Maabara kwa shule za Sekondari za Kata limeingia kwenye hatua nzito baada ya mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza kuiacha ofisi yake na kuhamia Wilaya ya Bagamoyo ili kuhakikisha agizo la Rais Dk Jakaya Kikwete la kila wilaya iwe imekamilisha ujenzi huo ifikapo Novemba 30 mwaka huu.
Sambamba na hilo mkuu huyo amewataka wakuu wa idara wa Wilaya hiyo kila mmoja kutokaa ofisini na kuchagua kata ya kwenda ili kusimamia ujenzi huo hadi ujenzi wa maabara...
10 years ago
Habarileo30 May
DC Mpwapwa apania ujenzi wa maabara
MKUU mpya wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Antony Mavunde ameapishwa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma huku akisema kipaumbele chake cha kwanza ni kuhakikisha ujenzi wa maabara unakamilika kwa wakati.
10 years ago
Habarileo27 Feb
RC: Hakuna visingizio ujenzi wa maabara
MKUU wa mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amewataka wakuu wa wilaya mkoani humo kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa maabara za sayansi kwenye kata ifikapo Machi mwaka huu.
10 years ago
Mtanzania11 Jun
Pinda: Ujenzi wa maabara palepale
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda amesema tarehe ya mwisho iliyotolewa na Serikali ya kusimamia ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari iko palepale na amewataka watendaji wa halmashauri na mikoa kuhakikisha wanatimiza agizo hilo.
Alitoa agizo hilo Mwanza jana alipozungumza na watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waratibu wa Elimu wa Wilaya na Mikoa waliohudhuria ufunguzi wa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Waziri Mkuu ambaye...
10 years ago
Habarileo08 Feb
Mikoa 6 taabani ujenzi wa maabara
MIKOA sita ‘imevurunda’ katika ujenzi wa maabara katika shule za sekondari baada ya kushindwa kufikia malengo. Ni mikoa mitatu pekee ndiyo imefanya vizuri kwa kuvuka nusu ya malengo.
10 years ago
Habarileo18 Dec
Pwani ujenzi wa maabara asilimia 80
WILAYA ya Kibaha mkoani Pwani imefikia asilimia 80 ya ujenzi wa maabara kwenye shule za sekondari na inatarajia kukamilisha ujenzi huo mwishoni mwa mwezi huu.