Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


MKUU WA UHAMIAJI KAGERA AFARIKI DUNIA

  Aliyekuwa Mkuu wa uhamiaji Mkoa Wa Kagera Pendo Buteghe amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Kagera alikokuwa akipatiwa   matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa kaimu mkuu wa uhamiaji Kagera Thomas Fush marehemu alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kushuka sukari mwilini.

Fush amesema kuwa kufuatia msiba huo mwongozo wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa na makao makuu ya uhamiaji umesubiriwa ili kujua taratibu za msiba na maziko

CCM Blog

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

Mwananchi

Monsinyori Bamanyisa afariki dunia Kagera

Aliyekuwa Katibu wa Kardinali wa kwanza Mwafrika, Mwadhama Laurean Rugambwa, Monsinyori Justinian Bamanyisa amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.

 

11 years ago

Tanzania Daima

Mkuu wa Mkoa wa Mara afariki dunia

MKUU wa Mkoa wa Mara,  John Tuppa, amefariki dunia jana akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Tarime. Taarifa za kifo chake zilitolewa kwa waandishi wa habari na Mkuu wa  Wilaya...

 

11 years ago

Habarileo

Mkuu wa Chuo UDSM afariki dunia

Marehemu Balozi Fulgence KazauraMKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Balozi Fulgence Kazaura, amefariki dunia juzi nchini India alikokuwa akitibiwa maradhi ya saratani.

 

10 years ago

GPL

WAZIRI MKUU WA ZAMANI IRELAND AFARIKI DUNIA

Albert Reynolds enzi za uhai wake. ALIYEWAHI kuwa Waziri Mkuu wa Ireland kwa miaka mitatu, Albert Reynolds amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81. Kiongozi huyo aliyewahi kuongoza Chama cha Fianna Fáil na kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel pia aliwahi kuwa Waziri wa Fedha (1988–91), Waziri wa Viwanda na Biashara (1987–88), Waziri wa Viwanda na Nishati (1982), Waziri wa Usafirishaji (1980–81) na Waziri wa...

 

5 years ago

CCM Blog

MKUU OFISI YA RAIS BUHARI AFARIKI DUNIA

Kiongozi wa ofisi ya rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amefariki baada ya kupatikana na virusi vya Corona.
Kupitia taarifa, ofisi ya Buhari imesema imesikitishwa na kifo cha Abba Kyari ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa katika utawala wa Rais huyo.Taarifa hiyo imesema kuwa marehemu alifariki jana Ijumaa kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Kyari aliyekuwa katika miaka ya sabini, ni mtu wa kwanza mwenye cheo cha juu nchini Nigeria kufariki kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Nchi hiyo yenye idadi kubwa...

 

11 years ago

Michuzi

TANZIA: MKUU WA WILAYA YA KALAMBO AFARIKI DUNIA

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo enzi za uhai wake Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari. Taratibu za mazishi zitatangazwa mapema mara baada ya kikao cha wanandugu. Tunatoa pole kwa wale wote walioguswa na msiba huu. Sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.(Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

 

11 years ago

GPL

MSIBA: MKUU WA WILAYA YA KALAMBO AFARIKI DUNIA

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a enzi za uhai wake . Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a amefariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na kisukari. Taratibu za mazishi zitatangazwa mapema mara baada ya kikao cha wanandugu. Tunatoa pole kwa wale wote walioguswa na msiba huu. Sisi tulimpenda...

 

10 years ago

Michuzi

TANZIA- MKUU WA MAGEREZA MKOA WA SHINYANGA AFARIKI DUNIA


                                                Marehemu SACP Aneth Laurent  enzi za uhai wake
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza - SACP Aneth Laurent kilichotokea jana Julai 30, 2015 katika Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza.Kamishna Jenerali wa Magereza anatoa pole kwa Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini, familia na wale wote...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani