Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


TANZIA- MKUU WA MAGEREZA MKOA WA SHINYANGA AFARIKI DUNIA


                                                Marehemu SACP Aneth Laurent  enzi za uhai wake
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza - SACP Aneth Laurent kilichotokea jana Julai 30, 2015 katika Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza.Kamishna Jenerali wa Magereza anatoa pole kwa Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini, familia na wale wote...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

GPL

TANZIA: MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA DODOMA, MARIAM MFAKI AFARIKI DUNIA

MBUNGE wa Viti Maalum, Mariam Mfaki (CCM), amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alipokuwa amelazwa. Marehemu amekuwa mbunge kwa vipindi vitatu, 2010 - 2015, 2005 - 2010 na 2000 - 2005. Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Mohammed Mfaki amesema mama yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani tangu mwaka 2012. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi. Amen. ...

 

11 years ago

Michuzi

TANZIA: MKUU WA WILAYA YA KALAMBO AFARIKI DUNIA

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo enzi za uhai wake Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari. Taratibu za mazishi zitatangazwa mapema mara baada ya kikao cha wanandugu. Tunatoa pole kwa wale wote walioguswa na msiba huu. Sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.(Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

 

10 years ago

Michuzi

TANZIA: ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA AFARIKI DUNIA

Hayati Dkt. Mohamed Mhita
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu (mstaafu) Dkt. Mohamed Mhita kilichotokea siku ya Jumatatu tarehe 06 Aprili 2015 katika hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mhita alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa iliyokuwa Idara Kuu ya Hali ya Hewa kwa kipindi cha miaka 8 kuanzia 1992 hadi 1999 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa kipindi cha miaka 9 kuanzia 1999...

 

11 years ago

Tanzania Daima

Mkuu wa Mkoa wa Mara afariki dunia

MKUU wa Mkoa wa Mara,  John Tuppa, amefariki dunia jana akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Tarime. Taarifa za kifo chake zilitolewa kwa waandishi wa habari na Mkuu wa  Wilaya...

 

11 years ago

GPL

BREAKING NEWS: MKUU WA MKOA WA MARA, GABRIEL TUPPA AFARIKI DUNIA

Mkuu wa mkoa wa Mara, Bw. John Gabriel Tuppa. MKUU wa mkoa wa Mara, Bw. John Gabriel Tuppa, amefariki dunia ghafla leo majira ya saa 4.30 asubuhi baada ya kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa shinikizo la damu akiwa wilaya ya Tarime mkoani Mara. Katibu tawala wa mkoa wa Mara, Bw. Benedict Ole Kuyan, amesema kuwa Bw. Tuppa kabla ya kifo chake leo asubuhi akiwa na afya njema alifika… ...

 

5 years ago

CCM Blog

TANZIA: MDOGO LOWASSA AFARIKI DUNIA


  Mdogo wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anayefahamika kwa kwa jina la Bernard Lowassa, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Aghakhan jijini Dar es salaam.


Mtoto wa Waziri Mkuu huyo Mstaafu Fred Lowassa amethibitisha hayo
"Ni kweli ndugu yetu Bernard lowassa amefariki yeye ni Baba yangu mdogo, na alikuwa amelazwa Aga Khan na hapa familia tunaenda hospitalini kwa ajili ya kukutana."- Amesema

 

9 years ago

GPL

TANZIA: MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI DUNIA

Mwanasiasa mashuhuri nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha DP Mch.Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msolwa kilichopo Chalinze mkoani Pwani asubuhi ya leo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema Mtikila amefariki majira ya saa 11:45 asubuhi ya leo katika kijiji...

 

5 years ago

CCM Blog

TANZIA: IDDI SIMBA AFARIKI DUNIA

   Aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika serikali ya awamu ya tatu, Iddi Simba amefariki dunia leo.
Taarifa zilizothibitishwa na mtoto wake, Sauda Simba Kilumanga zinasema Iddi Simba amefariki katika Hospitali ya JKCI alipokuwa akipatiwa matibabu.

 

10 years ago

GPL

TANZIA: ABDUL BONGE AFARIKI DUNIA

Abdul Bonge enzi za uhai wake. ALIYEWAHI kuwa Meneja wa wasanii na mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. Chanzo cha kifo cha Abdul Bonge bado hakijafahamika ila msiba upo Manzese Tip Top. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani