Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Mwanasheria Mkuu wa Serikali ajiuzulu

werema

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (pichani) amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake...

Dewji Blog

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

BBCSwahili

Mwanasheria Mkuu wa Tanzania ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Jaji Frederick Werema amejiuzulu siku ya jumanne kufuatia kashfa ya ESCROW aliyohusishwa.

 

10 years ago

GPL

MWANASHERIA MKUU WA SEREKALI, JAJI WEREMA AJIUZULU

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema (pichani) leo amejiuzulu nafasi yake na tayari amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Kikwete. Rais Kikwete asema amepokea barua yake na kumshukuru kwa ushirikiano aliouonyesha katika kipindi cha utumishi wake.…

 

9 years ago

Michuzi

JK ATEUA WAKUU WA MIKOA WAWILI, MGANGA MKUU WA SERIKALI, NAIBU MWANASHERIA MKUU NA MTENDAJI MKUU WA NDC


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu wawili wapya wa mikoa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wakuu wa Mikoa ambao wanawania ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa katika uteuzi wake, Rais Kikwete amemteua Ndugu Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Ndugu Jordan Rugimbana kuwa Mkuu...

 

9 years ago

StarTV

Rais Magufuli ateua Mwanasheria mkuu wa Serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli ameanza kazi rasmi mara baada ya kuapishwa, ambapo tayari amemteua John Mcheche Masaju kuwa mwanasheria mkuu wa serikali.

Pamoja na uteuzi huo, Rais Dr. Magufuli ameitisha bunge, na kuagiza kukutana November 17, wakati ambapo pia anatarajiwa kuwasilisha jina la atakayemkusudia kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano.

 Mapema jana, Rais Dokta Magufuli ameapishwa rasmi kwenye uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam, tukio...

 

9 years ago

Mwananchi

Masaju aapishwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)

Rais Dk John Magufuli amemuapisha George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu mjini Dar es Salaam.

 

10 years ago

Vijimambo

Rais ateua Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya

Bwana George Mcheche Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya...

 

9 years ago

Mwananchi

Magufuli aanza kazi, amteua mwanasheria mkuu wa serikali

Saa chache baada ya kuapishwa kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano, Dk John Magufuli amemteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali.

 

9 years ago

Michuzi

Mwanasheria Mkuu wa Serikali alia na mtuhumiwa wa madawa ya kulevya

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amewasilisha waraka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam akitaka kushikiliwa na kuzuiwa kwa mali zote za mtuhumiwa wa madawa ya kulevya, aliyejulikana kwa jina la Muharami Abdallah, maarufu kwa jina la Chonji na mkewe, Mwalibora Nyanguri kuhamisha umiliki, kupangisha au kuombea mikopo.
Maombi hayo dhidi ya Muharami na mkewe yaliwasilishwa kwa hati ya dharura mahakamani hapo Septemba 13, mwaka huu mbele ya Jaji Wilfred...

 

10 years ago

GPL

RAIS KIKWETE AMWAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI IKULU DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha George Mcheche, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akisaini nyaraka wakati wa hafla fupi ya kumwapisha, George Mcheche, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwenye hafla hiyo… ...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani