Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


NHIF yapunguza uhaba wa mashuka hospitali ya Singida

HOSPITALI ya Mkoa wa Singida inakabiliwa na uhaba mkubwa wa mashuka hali inayosababisha baadhi ya wagonjwa kutumia mashuka yao binafsi wakati wote wanapokuwa wamelazwa hospitalini hapo.

habarileo

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Dewji Blog

NHIF yakabidhi msaada wa mashuka 200 kwa hospitali ya mkoa mjini Singida

DSC00136

Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Singida, Alli Amanzi msaada wa mashuka 200 kwa ajili ya hospital ya mkoa mjini hapa.(Picha na Nathaniel Limu).

DSC00132

Mkuu wa wilaya ya Singida,Alli Amanzi (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Singida, Agnes Chaki (katikati) muda mfupi kabla Meneja NHIF hajakabidhi mashuka 200 kwa hospitali ya mkoa mjini hapa.Kushoto ni Afisa uthibiti ubora wa huduma NHIF mkoani...

 

10 years ago

GPL

NHIF YAKABIDHI MSAADA WA MASHUKA 200 KWA HOSPITALI YA MKOA MJINI SINGIDA‏

Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Singida, Alli Amanzi msaada wa mashuka 200 kwa ajili ya hospital ya mkoa mjini hapa.(Picha na Nathaniel Limu). Mkuu wa wilaya ya Singida, Alli Amanzi (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Singida, Agnes Chaki (katikati) muda mfupi kabla Meneja NHIF hajakabidhi mashuka 200 kwa hospitali ya mkoa...

 

10 years ago

Michuzi

NHIF yakabidhi mashuka hospitali ya wilaya

Na Editha Karlo,wa bog ya jamii KigomaMFUKO wa Taifa wa bima ya afya umetoa jumla ya mashuka 100 kwa hospitali ya wilaya ya Kibondo mkoani kigoma ili kukabiliana na upungufu wa mashuka unaoikabili hospitali hiyo.
Akikabidhi mashuka hayo kwa uongozi wa hospitali ya wilaya ya Kibondo, meneja wa NHIF mkoa kigoma,Elius Odhiambo alisema kuwa kutolewa kwa mashuka hayo ni sehemu ya mpango wa mfuko huo katika kuboresha utoaji huduma katika sekta ya afya.
Odhiambo alisema kuwa mashuka hayo yaliyotolewa...

 

10 years ago

Michuzi

NHIF yatoa msaada wa mashuka Hospitali ya Vijibweni

 Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu Dk. Frank Lekey akikabidhi mashuka kwa Muuguzi wa Hospitali ya Vijibweni Maimuna Mwaya. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekabidhi jumla ya mashuka 150 katika Hospitali hiyo ambayo iilikuwa na uhaba mkubwa wa mashuka. Mganga Mfawidhi Emanuel Bwana akitandika kitanda kwa shula la NHIF ambalo ni moja ya mashuka yaliyokabidhiwa hospitalini hapo.  Mganga Mfawidhi Emanuel Bwana akielezea huduma zinazotolewa hospitalini hapo na kuushukuru Mfuko kwa msaada wa...

 

10 years ago

Michuzi

NHIF WATOA MSAADA WA MASHUKA 120 HOSPITALI YA MANISPAA YA TEMEKE

 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wa mkoa wa Temeke (NHIF),Constantine Makala akieleza jambo wakati wa kukabidhi mashuka 120 katika hospitali ya Temeke leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk.Edwin Muhondezi. Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wa mkoa waTemeke (NHIF), Constantine Makala akimuwakilisha kaimu  Mkurungenzi Mkuu wa (NHIF) wa mkoa wa Temeke kumkabidhi msaada wa mashuka 120 Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke Edwin Muhondezi...

 

9 years ago

Michuzi

NHIF YATOA MSAADA WA MASHUKA 100 HOSPITALI YA MJI WA BABATI

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela (kulia) akipokea moja kati ya msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kutumiwa na wagonjwa wa hospitali ya mji wa Babati (Mrara), anayemkabidhi mashuka hayo ni Meneja wa NHIF Mkoani humo, Isaya Shekifu. Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu akizungumza mara baada ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Babati Crispin Meela mashuka 100 waliyotoa msaada...

 

9 years ago

StarTV

Wagonjwa vituo vya afya Tanga kutumia mashuka yao kutokana na uhaba wa mashuka

Uhaba wa mashuka katika vituo vya afya mkoani Tanga umesababisha baadhi ya wagonjwa kutumia mashuka yao binafsi jambo ambalo halikubaliki kiafya.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza amekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambalo limekuwa likisababisha usumbufu kwa wagonjwa wanaohudumiwa katika vituo hivyo.

Mahiza amesema hayo wakati akipokea msaada wa mashuka kutoka Mfuko wa Bima ya Afya NHIF kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo katika mkoa wa Tanga.

 Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga inajumla ya...

 

9 years ago

StarTV

Wagonjwa hospitali ya mkoa Singida watumia mashuka yao

Wagonjwa wanaolazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida wapo hatarini kupata maambukizi ya magonjwa mengine kutokana na kutumia mashuka wanayotoa nyumbani na kujifunika bila kuyafanyia usafi suala ambali ni kinyume na taratibu na kanuni za afya.

Hii ni kutokana na Hospitali hiyo kuwa na mashuka  235 pekee kati ya 2,500 yanayohitajika, kiwango ambacho ni chini ya asilimia 10 ya mahitaji hivyo kuulazimu uongozi kutoa ruksa kwa kila mgonjwa anayelazwa kwenda na shuka lake.

Wagonjwa mbalimbali...

 

9 years ago

Michuzi

NHIF Mkoa wa Manyara watoa msaada wa mashuka 100 kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara).

 Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela (kulia) akipokea moja kati ya msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kutumiwa na wagonjwa wa hospitali ya mji wa Babati (Mrara) anayemkabidhi ni meneja wa NHIF Mkoani humo, Isaya Shekifu. Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela (kulia) akipokea msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kutumiwa na wagonjwa wa hospitali ya mji...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani