Nyumba 30 zabomolewa na mvua Mara
Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali, imesababisha nyumba zaidi ya 30 kuanguka, ng’ombe saba kufa katika vitongoji vya Maganana na Mgenda Msirori katika Kijiji cha Gusuhi, Kata ya Nyambureti Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
Mwananchi
Habari Zinazoendana
11 years ago
Habarileo08 Aug
Nyumba za Mchungaji Rwakatare zabomolewa
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Makazi jana imebomoa nyumba nne zilizojengwa ndani ya kiwanja namba 314 zilichopo eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam zinazomilikiwa na Mchungaji Getrude Rwakatare kwa tuhuma kuwa alivamia eneo hilo.
9 years ago
Mwananchi18 Dec
Nyumba 100 zabomolewa Msimbazi
9 years ago
Global Publishers17 Dec
Nyumba zilizopo kwenye Bonde la Mkwajuni, Dar zabomolewa
Wakazi waishio katika Bonde la Mkwajuni leo wamebomolewa nyumba zao ikiwa ni mwendelezo wa bomoabomoa inayoendelea katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi waliokubwa na kadhia hiyo wamepaza sauti zao juu ya kuvunjiwa nyumba zao huku wakilalamika kuwa hawakupewa taarifa yoyote ya kuwataka wahame eneo hilo kutoka uongozi wa serikali ya mtaa huo.
9 years ago
StarTV03 Dec
Ukamilishaji jengo la biashara Mutukula wachelewa kutokana na mvua za mara kwa mara
Ujenzi wa jengo la kisasa la biashara linalojengwa na shirika la Nyumba la Taifa katika mpaka wa Mutukula mkoani Kagera umechelewa kukamilika kutokana na mvua za mara kwa mara ambazo zimekuwa kikwazo katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo linalokadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni tatu nukta nne tano hadi litakapokamilika.
Awali ujenzi wa jengo hilo ulipangwa kukamilika Desemba mwaka huu lakini kutokana na mvua za mara kwa mara, jengo hilo sasa linatarajiwa kukamilika...
10 years ago
Mtanzania05 Mar
Maafa Shinyanga *Barafu yafunika kijiji, watu 42 wafariki dunia *Zaidi ya 91 wajeruhiwa, mamia wasombwa na maji *Nyumba zabomolewa, mifugo mingi nayo yafa
Paul Kayanda na Kadama Malunde, Kahama
WATU 42 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 91 wamejeruhiwa vibaya baada ya mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali kunyesha katika Kijiji cha Mwakata, Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga.
Pamoja na vifo hivyo, nyumba za makazi na majengo ya taasisi mbalimbali, yamebomolewa na mafuriko yaliyosababishwa mawe kusambaa kijiji kizima.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya, aliiambia MTANZANIA kwa simu jana kwamba zaidi ya kaya 100...
11 years ago
Mwananchi16 Feb
Mvua yaua, yaezua nyumba 62
11 years ago
Habarileo20 Apr
Mvua yabomoa nyumba 300 Rorya
NYUMBA 300 katika kata tano wilayani Rorya, zimeharibiwa na mvua iliyonyesha mwishoni mwa wiki.
11 years ago
Habarileo13 Apr
Mvua yaua watu, nyumba zasombwa
MVUA iliyonyesha juzi na jana, ikiambatana na upepo mkali katika mikoa mbalimbali nchini, imeleta madhara na kusababisha vifo vya watu kadhaa. Jijini Dar es Salaam, nyumba nyingi zimebomolewa na kuzingirwa na maji, na miundombinu imekatika, ikiwemo kufunikwa kwa madaraja muhimu na adha za kila aina.
11 years ago
Habarileo14 Feb
Mvua yaua mmoja, yaezua nyumba 85
MVUA zimeleta maafa mkoani Kilimanjaro baada ya mtu mmoja kufariki dunia sanjari na nyumba zaidi ya 85 kuezuliwa mapaa. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga, alisema kaya takribani 85 zimekosa makazi. Aidha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibohehe, na Shule ya Msingi Kishare wamekosa pa kusomea kutokana na baadhi ya madarasa kuezuliwa mapaa kwa upepo.