Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


RC MAKONDA ATANGAZA KUANZIA JUMATATU WANANCHI WOTE WANAOTOKA MAJUMBANI LAZIMA WAWE WAMEVAA BARAKOA

*Pia ataka kila familia ijadili inavyoweza kukabiliana na virusi vya Corona


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WANANCHI wa Jiji la Dar es Salaam hasa wale ambao wanatoka na kwenda kwenye shughuli mbalimbali wanatakiwa kuvaa barakoa kuanzia Jumatatu ya Aprili 20, mwaka huu kama hatua ya kukabiliana na virusi vya Corona na atakayekaidi atachukuliwa hatua kali.

Akizungumza leo Aprili 18, 2020 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa kuanzia Jumatatu watu wa Jiji hilo watatakiwa kuvaa...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

5 years ago

Michuzi

Abiria wanaotoka mikoa iliyoathirika kukaa Karantini Rukwa, wananchi wakitakiwa kuvaa barakoa

Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo. 
KATIKA harakati za kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (COVID – 19) Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo ametoa maelekezo kwa wananchi wa mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanavaa barakoa wanapokuwa katika mikusanyiko pamoja na maeneo yao ya kibiashara hasa kwa wale wanaohusika na kutoa huduma kwa jamii huku akivitaka vyombo husika kuhakikisha abiria wote wanaotoka katika maeneo yaliyoathirika ndani ya nchi kuingia...

 

5 years ago

CCM Blog

KUINGIA BUGANDO KUANZIA LEO LAZIMA KUVAA BARAKOA


  Kuanzia leo Aprili 24, 2020, mtu yeyote yule, wakiwemo wagonjwa ama ndugu za wagonjwa atakayeingia katika Hospitali ya Bugando  jijini Mwanza, atatakiwa kuvaa barakoa na kuirejesha getini kabla ya kutoka, ikiwa ni hatua ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.

 

5 years ago

Michuzi

RC MAKONDA ATANGAZA DAWA KWA WAKANDARASI WANAOKIUKA TARATIBU ZA MIKATABA * RC Makonda asema hakuna mgonjwa wa Covid 19, awataka wananchi kufuata maelekezo Na Leandra Gabriel, Michuzi TV MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza kamati ya w

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya  kamati ya watu 13 kutoka Serikali na sekta binafsi ambao watapitia mikataba yote ya miradi mbalimbali iliyosainiwa mkoa wa Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa globu ya jamii)
* RC Makonda asema hakuna mgonjwa wa Covid 19, awataka wananchi kufuata maelekezo
Na Leandra Gabriel, Michuzi TVMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza kamati ya watu 13 kutoka Serikali na sekta binafsi ambao...

 

5 years ago

Michuzi

WANANCHI DAR WAITIKIA AGIZO LA MAKONDA...BARAKOA KILA MAHALI


Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

WAKAZI wa Jiji la Dar es  Salaam wameitikia mwito wa Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda wa kuvaa barakoa kama hatua mojawapo ya kukabiliana na virusi vya Corona.

Juzi Makonda alitangaza kwamba kuanzia Jumatatu (leo) wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam watatakiwa kuvaa barakoa na kwamba kwa wale ambao watakaidi hatua za kisheria zitachukuliwa.Hata hivyo asilimia kubwa ya wananchi wameitikia mwito huo kwani kila kona ya Jiji hilo wamevaa barakoa.

Michuzi TV na Michuzi Blog...

 

5 years ago

CCM Blog

RAIS WA UGANDA: KUVAA BARAKOA NI LAZIMA SIO HIYARI

    Kila mtu anapotoka nyumbani ni lazima avae barakoa , sio hiari kuvaa barakoa ni lazima ,tujikinge na corona , naambiwa kuna watu wameanza kunyanyasana hata kwenye familia , wanafamilia wengine hawataki kukaa pamoja , niwakumbushe tu familia ndio kila kitu maishani.

 

5 years ago

Michuzi

UGANDA YALEGEZA MASHARTI YA 'LOCKDOWN', YATANGAZA KUVAA BARAKOA NI LAZIMA

Rais Yoweri Museveni ametangaza kuwa kuvaa barakoa ni jambo la lazima nchini humo kuanzia leo katika kipindi hiki ambacho marufuku ya kutotoka nje inalegezwa.

Hatua hiyo ilitangazwa Jumatatu usiku ambapo rais Museveni alihutubia taifa baada ya kumaliza siku 35 za marufuku ya kutotoka nje ama 'lockdown'.

Museveni amesema watu wanaweza kuvalia mpaka barakoa ambazo zimeshonwa kienyeji na vitambaa.

Hata hivyo, kumekuwa na mashaka kutoka kwa wataalamu wa afya juu ya ufnisi wa barakoa za kutengenezwa...

 

5 years ago

CCM Blog

MUFTI MKUU SAUDI ARABIA ATANGAZA TARAWEHE NA IDDI KUSWALIWA MAJUMBANI

  Mufti Mkuu wa Saudi Arabia, Sheikh Abdulaziz Al-Sheikh, amesema kuwa sala zote kwenye mwezi wa Ramadhan na Eid-al-Fitr zitapaswa kuswaliwa majumbani, endapo janga la kirusi cha corona litaendelea, hii ikiwa fatwa ya karibuni kabisa kutolewa na kiongozi huyo wa juu wa dini ya Kiislamu nchini humo.

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan unaanza wiki ijayo, katika wakati ambapo maradhi ya COVID-19 yakipamba moto. Katikati ya mwezi uliopita wa Machi, Saudi Arabia ilifunga misikiti yote kuzuwia...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani