Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Serikali yaanza kusambaza Katiba Inayopendekezwa

Waziri Migiro

Waziri Migiro akiongea na baadhi ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Na Mwandishi Wetu

Serikali imeanza kusambaza nakala milioni mbili za Katiba Inayopendekezwa nchini kote ili kuwawezesha wananchi kuisoma na kushiriki katika Kura ya Maoni iliyopangwa kufanyika tarehe 30 Aprili mwaka huu.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro amesema leo (Jumatano, Februari 11, 2015) jijini Dar es Salaam kuwa kati ya nakala hizo zilizochapwa jijini Dar es Salaam, nakala 1,800,000...

Dewji Blog

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mwananchi

Serikali yaanza kugawa nakala milioni mbili Katiba inayopendekezwa

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro amesema kila kata nchini itapata nakala 300 za Katiba Inayopendekezwa ili kuwawezesha wananchi  kuisoma na kushiriki katika Kura ya Maoni iliyopangwa kufanyika Aprili 30, mwaka huu.

 

10 years ago

Mtanzania

Katiba inayopendekezwa yaanza kusambazwa

27Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SERIKALI imeanza kusambaza nakala milioni mbili za Katiba inayopendekezwa nchini kote ili kuwawezesha wananchi kuisoma na kushiriki katika kura ya maoni iliyopangwa kufanyika Aprili 30.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa kati ya nakala hizo zilizochapwa, 1,800,000 zinasambazwa Tanzania Bara na 200,000 upande wa Zanzibar.
Dk. Migiro alisema hadi kufikia juzi, jumla ya nakala 707,140 zilikuwa zimesambazwa...

 

11 years ago

Habarileo

Serikali yaanza kusambaza kompyuta vyuoni

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali kwa sasa imeanza kusambaza kompyuta katika vyuo vikuu nchini kwa lengo la kuboresha elimu kwa wanafunzi. Pia, amesema baadaye Serikali itaanza kusambaza kompyuta ndogo zinazobeba vitabu kidijitali, maarufu kama tabuleti (tablets) kwa wanafunzi.

 

10 years ago

Mwananchi

MSD yaanza kusambaza dawa

>Bohari Kuu ya Dawa (MSD) imeanza kusambaza dawa katika hospitali mbalimbali nchini, baada ya kupokea kiasi cha Sh20 bilioni ambazo ni sehemu ya malipo ya deni linaloidai Serikali.

 

10 years ago

Mwananchi

Madaraka ya Bunge sasa, katika Rasimu ya Katiba Mpya na Katiba inayopendekezwa

Natambua kwamba bado tuna joto la sakata la “escrow” ambalo hata baada ya Mkuu wa Nchi Rais Jakaya Kikwete kulifafanua na hata kama hujui kusoma upepo kiasi gani utakuwa umegundua na utaungana nami kwamba bado wananchi wamegawika kabisa.

 

10 years ago

GPL

KATIBA INAYOPENDEKEZWA NI KIVULI CHA ‘KATIBA YA NYERERE’

Tundu Lisu. UKITAKA kuwaudhi Watanzania wengi – wasomi na wajinga, wafupi na warefu, walevi na wasiotumia vileo  – unachotakiwa kufanya ni kutaja makosa aliyoyafanya Rais wa Kwanza wa Tanzania, Julius Kambarage Nyerere akiwa madarakani.  Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, katika mijadala ya kuweka mambo sawa kitaifa, aliposema: “Nyerere hakuwa  Mungu” akimaanisha yaliyofanywa na kusemwa...

 

10 years ago

GPL

MH. CHENGE AWASILISHA RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba Mhe. Andrew Chenge (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe. Samuel Sitta (kushoto) Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi cha Bunge hilo. Kamati ya Uandishi imemaliza kazi ya kuandaa Rasimu hiyo na inatarajiwa kusomwa Bungeni siku ya kesho. Makabidhiano yakiendelea.… ...

 

10 years ago

GPL

BUNGE MAALUM LA KATIBA LAPITISHA RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta hivi punde ametangaza rasmi kupitisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa baada ya matokeo…

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani