Video ya Shaa ‘Toba’ iliyoongozwa na Campos kutambulishwa na MTV Base Jumatatu Nov.23
Ile video mpya ya Shaa aka Malkia wa Uswazi, ‘Toba’ aliyoshoot na muongozaji Justin Campos wa Afrika Kusini na kukaa nayo ndani kwa muda mrefu, sasa itatambulishwa Jumatatu ya November 23.
Video hiyo itaoneshwa kwa mara ya kwanza na kituo cha MTV Base kupitia segement yao ya kutambulisha video mpya ‘Spanking New’, saa 12 za jioni saa za Afrika Mashariki.
Wimbo na video hiyo ni muendelezo wa kazi za Shaa kwenye mkataba wake na Said Fella pamoja na Babu Tale ambao pia ndio walihusika na...
Bongo5
Habari Zinazoendana
9 years ago
Bongo523 Nov
Video: Tazama kionjo cha video mpya ya Shaa ‘Toba’ iliyoongozwa na Justin Campos

Masaa machache kabla video ya wimbo mpya wa Shaa ‘Toba’ haijatambulishwa rasmi kupitia MTV Base, muimbaji huyo ametupa kionjo kidogo.
Video hiyo imeongozwa na director wa Afrika Kusini, Justin Campos. Usikose kuitazama leo jioni (Nov.23) saa 12 kamili kupitia MTV Base ‘Spanking New’
Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!
9 years ago
Bongo510 Nov
Video ya wimbo mpya wa Joh Makini ft. AKA ‘Don’t Bother’kutambulishwa MTV Base (Nov.10)

Baada ya Nikki Wa Pili wa Weusi kutambulisha wimbo wake mpya ‘Baba Swalehe’ Ijumaa iliyopita, sasa ni zamu ya kaka yake Joh Makini kuwaonesha mashabiki wake wa Tanzania na Afrika kwa ujumla kile alichoenda kufanya Afrika Kusini miezi kadhaa iliyopita.
Video ya wimbo mpya wa Joh Makini aliomshirikisha rapper wa Afrika Kusini ‘AKA’ itatambulishwa kwa mara ya kwanza leo (Nov. 10) saa 12 jioni (saa za Afrika Mashariki) na kituo cha kimataifa cha MTV Base.
‘Don’t Bother’ imetayarishwa na...
9 years ago
Bongo520 Nov
Shaa kuachia video iliyoongozwa na Justin Campos ‘soon’

Hivi karibuni wasanii wamekuwa na tabia ya kushoot video kali na kukaa nazo ndani bila kusema chochote.
Shaa ni mmoja wapo. Ukimya wake haumaanishi kuwa hakuna vitu vikubwa vinavyofanyika nyuma ya pazia. Muimbaji huyo miezi kadhaa iliyopita alisafiri hadi Afrika Kusini kwenda kushoot video ya wimbo wake na muongozaji aliyejikusanyia sifa Afrika, Justin Campos.
Mke wa Justin, Candice, amepost picha ya screeshot kwenye Instagram kutoka kwenye kile kinachoonekana ni video ya wimbo huo uitwao...
10 years ago
Bongo502 Sep
Video ya Yamoto Band ‘Cheza Kwa Madoido’ kutambulishwa MTV Base (Sept 2)
10 years ago
Bongo523 Apr
Video mpya ya Joh Makini ‘Nusu Nusu’ kutambulishwa ‘Exclusive’ na MTV Base Ijumaa (April 24)
9 years ago
Bongo517 Dec
Wimbo mpya wa Chege aliomshirikisha Runtown wa Nigeria kutambulishwa leo (Dec.17) na MTV Base

Ni muda mrefu umepita toka msanii kutoka TMK, Chege Chigunda aanze kuzunguzia kuwa anafanya collabo na msanii wa Nigeria, Runtown na Uhuru wa Afrika Kusini – Sweety Sweety, na hatimaye sasa video ya wimbo huo iliyofanyika Afrika Kusini hivi karibuni itatambulishwa kwa mara ya kwanza kupitia MTV Base.
Video hiyo iliyoongozwa na Justin Campos wa Gorilla Films itaoneshwa kwenye Spanking New ya MTV Base Ahamisi Dec. 17, 2015 saa 12 jioni (saa za Afrika Mashariki).
Chege anaongezeka kwenye...
9 years ago
Mtanzania26 Nov
Shaa ashangazwa na wimbo wake wa ‘Toba’
NA CHRISTOPHER MSEKENA
STAA wa Bongo Fleva, Sara Kaisi ‘Shaa’, ameibuka na kudai kwamba anashangaa video yake ya wimbo wa ‘Toba’ kupokelewa vizuri na kwa haraka licha ya kurekodi wimbo huo miaka miwili iliyopita.
Akiuzungumzia wimbo huo, Shaa alisema kuwa wakati anaandika wimbo huo alilenga maisha ya miaka ya mbele ndiyo maana alipoutoa ukapata nafasi kubwa ya kuchezwa kwenye redio na runinga kubwa ikiwemo MTV Base.
“Sikutarajia kama ungefanya vizuri kwa sababu wimbo wenyewe umeandaliwa na...
9 years ago
Bongo528 Nov
Wimbo mpya wa Shaa ‘Toba’ umeandikwa na muimbaji wa ‘Mchumba’ H.Mbizo

Aliyeandika wimbo mpya wa Shaa ‘Toba’ uliotoka wiki hii, ni msanii wa muda mrefu aitwaye H.Mbizo.
H.Mbizo ni msanii aliyewahi kufanya vizuri miaka ya nyuma na wimbo wake uitwao ‘Mchumba’.
Said Fella ameiambia Bongo5 kuwa Mbizo aliuandika wimbo wote miaka miwili iliyopita na kutayarishwa na producer wa Nigeria aitwaye Big H.
Ameongeza kuwa wengine waliohusika na utayarishaji wa wimbo huo ni producer Shirko pamoja na shemeji Master Jay.
Katika hatua nyingine Shaa kupitia gazeti la Mtanzania...
10 years ago
Mtanzania12 Aug
Video ya Jux yachezwa MTV Base
NA ELLY MHAGAMA (TUDARCO)
MSANII wa Bongo Fleva, Juma Mussa (Jux) ametambulisha video ya wimbo wake mpya aliouita ‘I m looking for you’ ambao picha za video yake imefanyika nchini Afrika Kusini.
Katika video hiyo aliyomshirikisha mwana hip hop, Joh Makini, ni ya kwanza kwa msanii huyo kuchezwa katika kituo cha kimataifa cha MTV Base.
Wimbo huo uliochezwa katika kituo hicho jana majira ya saa 12, video yake imeandaliwa na muongozaji kutoka Afrika Kusini, Justin Compos wa Gorilla Films huku...