Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Wabunge wambeba Lowassa mbio urais

 Wakutana Dodoma, wamshawishi achukue fomu , Wamo kutoka Dar, Tanga, Singida, Ruvuma, KageraMbio za kuusaka urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimezidi kupamba moto baada ya kundi la wabunge wapatao 150 kujitokeza hadharani na kueleza kumuunga mkono mmoja wa wanaotajwa kuwa wagombea, Edward Lowassa, wakimtaka kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Hali hiyo inajitokeza wakati wa Mkutano wa Bunge wa 18 ukihitimishwa mwishoni mwa wiki na kubakia miwili tu Bunge la 10 kufikia tamati, hivyo...

Vijimambo

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Vijimambo

Siri Imefichuka:Rais Kikwete “Abariki” Mbio za Urais wa Lowassa


SIRI imefichuka. Mbio za Edward Lowassa, kusaka urais kwa udi na uvumba, zimebarikiwa kwa asilimia 100 na Rais Jakaya Kikwete.Lowassa amekutana na Kikwete mara kadhaa na kufunga makubaliano ya siri yanayolenga kumsaidia yeye kuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Yote yanayofanywa na Edward (Lowassa), yamebarikiwa na Kikwete. Bila hivyo, Lowassa asingekuwa na ubavu wa kufanya anachokitenda,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya serikali.Kikwete ndiye Mwenyekiti wa Taifa...

 

10 years ago

Mtanzania

Upinzani wambeba Prof. Mwandosya urais 2015

Mwandosya-MarkNA GORDON KALULUNGA, MBEYA
VIONGOZI wa Chama cha NCCR-Mageuzi na TADEA mkoani hapa, wamemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwamba ni mtu mwadilifu.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Mbeya, viongozi hao walisema wamechoshwa na tetesi na minong’ono iliyopo mitaani kuwa atawania nafasi hiyo huku yeye akiwa amekaa kimya bila kukata kiu ya wafuasi wake ndani na nje ya CCM.
Kamishna wa...

 

10 years ago

Vijimambo

MBIO ZA URAIS

Butiama. Mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Charles Makongoro, ametangaza nia ya kuwania urais, akisema anaomba kibali kuisaidia CCM iache rushwa, kuparaganyika na atakapoingia madarakani, ili asiwaangushe Watanzania, anahitaji chama imara kisicho na shaka kama ilivyo sasa.Akitangaza nia hiyo nyumbani kwao Mwitongo, Butiama jana, Makongoro alisema kutokana na CCM “kubakwa na vibaka,” inawavunja moyo wanachama na inawakatisha tamaa Watanzania, hivyo inahitaji kiongozi...

 

10 years ago

Mtanzania

Mbio urais CCM

Khamis Mkotya na Debora Sanja, Dodoma

HATIMAYE mbio za urais, ubunge, udiwani na uwakilishi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimeanza rasmi, baada ya chama hicho kutangaza ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu.
Ratiba hiyo inaonyesha fomu za wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar zitaanza kutolewa Juni 3 na kurejeshwa Julai 2, mwaka huu, saa kumi jioni.
Kuhusu nafasi ya ubunge, udiwani na uwakilishi, wagombea wa nafasi hiyo wanatakiwa kuchukua fomu kuanzia Julai 15...

 

11 years ago

Uhuru Newspaper

MBIO ZA URAIS 2015



 Ngeleja naye afunguka
NA PETER KATULANDA, MWANZA
WAKATI vijana wakiendelea kupigiwa upatu katika harakati za kuwania urais katika uchaguzi mkuu mwakani, Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja, ameibuka na kuweka mambo hadharani.

Ngeleja, ambaye amewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini na miongoni mwa wanasiasa vijana wanaotajwa kuwa wanatosha kwenye nafasi hiyo, amesema ni mapenzi ya Mungu ndiyo yatamwongoza kuwania nafasi hiyo au kuendelea na ubunge.
“Kwa sasa naendelea kutii maagizo ya...

 

10 years ago

Tanzania Daima

Pinda: Nimeanza mbio za urais

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amefanya kile alichokifanya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, kwa kutangaza nia ya kuwania urais mwaka 2015, akiwa jijini London nchini Uingereza. Pinda...

 

10 years ago

Habarileo

Mkulima anogesha mbio za urais

MKULIMA kutoka Kasulu mkoani Kigoma, Eldeforce Bilohe akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu.MKULIMA kutoka Kasulu mkoani Kigoma, Eldeforce Bilohe (43) jana alichukua fomu za kuwania urais na kusema kuwa kati ya wagombea 27 ambao wamejitokeza haoni kama kuna mgombea ambaye ni tishio kwake.

 

9 years ago

StarTV

Mbio za urais visiwani Zanzibar

hamad JOTO la kuwania urais wa Zanzibar limezidi kupanda huku mgombe wa nafasi hiyo kupitia Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamesd akijitosa kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.

Hamad ametamba kuwa anatarajia kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kuanzisha shirika jipya la ndege la Zanzibar iwapo wananchi watampigia kura kuwa Rais mpya katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Hamad alitoa msimamo huo jana mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kuwania urais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchguzi...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani