Wahisani wakubali kuchangia bajeti
SHAMIMU MATTAKA (DACICO)
HATUA zilizochukuliwa na serikali dhidi ya waliochota zaidi ya Sh bilioni 200 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow zimesaidia Tanzania kukubaliwa kupewa Sh bilioni 71 na wahisani wa Maendeleo katika bajeti ijayo ya 2015/2016.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alisema Dar es Salaam jana kwamba wahisani hao wamefikia hatua hiyo baada ya kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali dhidi ya watuhumiwa.
“Baada ya suala hilo Tanzania ilikuwa katika sura ambayo si nzuri lakini...
Mtanzania
Habari Zinazoendana
11 years ago
Tanzania Daima26 May
Wahisani wajitoa kuchangia mapambano ya Ukimwi
KASI ya maambukizi ya Ukimwi Wilaya ya Moshi Vijijini imetajwa kuongezeka kutokana na mashirika yasiyo ya kiserikali kuacha kuwasaidia watoto yatima kutokana na nchi wahisani kuyafutia misaada mashirika hayo. Akizungumza...
9 years ago
Global Publishers29 Dec
Tanzania ya Magufuli inaweza kusimamia bajeti bila wahisani
Rais wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli.
Kasi aliyoingia nayo madarakani Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli imeendelea kuwa gumzo kila kona, ndani na nje ya nchi huku wadau wengi wakionesha kumpongeza hasa katika suala zima la kuhakikisha serikali yake inakusanya kodi kwa wingi na kuziba mianya yote ya ‘upigaji’ wa mali za umma uliokuwa umekithiri.
Ipo wazi kwamba mataifa yote makubwa yaliyoendelea duniani, ikiwemo Marekani na nchi nyingine za Ulaya,...
11 years ago
Dewji Blog21 May
Japan yaahidi kuendelea kuchangia Bajeti ya Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu Kiongozi wa Japan, Yoshihiro Suga, wakati alipofika ofisini kwake Jijini Tokyo Japan leo Mei 21, 2014, akiwa katika ziara ya kikazi. (Picha na OMR).
Mwandishi Maalum, Tokyo
Serikali ya Japan imeelezea nia yake ya kuendelea kuchangia bajeti ya Tanzania na kufafanua kuwa, inafanya hivyo kwa kutambua kuwa Tanzania ni mshirika mkubwa wa maendeleo na kwamba ni nchi yenye kutia...
10 years ago
BBCSwahili23 Dec
Wahisani wafurahishwa na hotuba ya :JK
11 years ago
BBCSwahili20 May
Wahisani kuijadili hali ya Sudan:K
10 years ago
Uhuru Newspaper11 Mar
Wahisani waanza kumwaga misaada
Wakunwa na hatua dhidi ya vigogo Escrow
NA MUSSA YUSUPH
NCHI na mashirika wahisani wameanza mchakato wa kutoa fedha za msaada wa bajeti walizozizuia, kutokana na sakata la uchotwaji wa fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, baada ya kuridhika na hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika.
Fedha zitakazotolewa ni sh. bilioni 922, ambazo ni sehemu ya asilimia tano zitakazotumika kusaidia bajeti, ambapo kabla ya kuzuliwa, asilimia 20 ya fedha hizo, zilikuwa zimekwishatolewa kwa serikali.
Akizungumza...
11 years ago
Habarileo06 Jun
Wahisani waanza kutekeleza ahadi
KILIO cha wabunge kuhusu baadhi ya wizara kukosa fedha kama zilivyoidhinishwa na Bunge katika Bajeti inayoisha, kimesikika ambapo mazungumzo kati ya Serikali na wahisani, yamezaa matunda kwa baadhi ya wahisani kukubali kutoa fedha hizo kabla la Juni 30, mwaka huu.
10 years ago
BBCSwahili24 Dec
Sahihisho:Wahisani bado wanaikaba Tanzania
10 years ago
Dewji Blog07 Nov
Waziri Pinda azishangaa nchi wahisani
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (pichani), amesema kuwa amesononeshwa na uamuzi wa wahisani kuikatia Serikali misaada ya sh trilioni moja kutokana na kashfa ya IPTL.
Pinda, alisema Serikali iko tayari kuwawajibisha watu wawili au zaidi watakaotajwa kuhusika kwenye kashfa ya kuchota fedha kwenye Akaunti Maalum ya Tegeta Escrow, zaidi ya sh bilioni 200, zilizohifadhiwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), lakini hakubaliani na uamuzi wa kukata misaada, kwani unaathiri watu wengi...