Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


WAKUU WA MIKOA YA MBEYA NA RUKWA WAMTEMBELEA MTOTO ALBINO ALIYEKATWA KIGANJA

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya, Dk. Mpoki Ulisubisya akiwaongozwa Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa kuelekea Wodini kumjulia hali Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi akiwa amelala kitandani akiendelea kupatiwa matibabu.Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stellah Manyanya akiwa anamwangalia kwa jicho la huruma Mtoto Baraka aliyekatwa...

Vijimambo

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mwananchi

Kiganja cha mtoto albino wa Rukwa chapatikana Mbozi

Kiganja cha mtoto Baraka Cosmas (6) mwenye ulemavu wa ngozi (albino) kilichokatwa Machi 8 kwenye Kijiji cha Kipeta, Sumbawanga Vijijini kimepatikana mwishoni mwa wiki wilayani Mbozi.

 

10 years ago

Mwananchi

Mtoto albino akatwa kiganja, jamii ifanye nini?

Ni masikitiko makubwa kwamba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi katika Kijiji cha Kipeta, Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa amejeruhiwa na watu wasiojulikana baada ya kukatwa kiganja cha mkono wa kulia. 

 

10 years ago

Michuzi

UJENZI WA BARABARA YA LAMI KUUNGANISHA MIKOA YA MBEYA NA RUKWA WAKAMILIKA, WAZIRI WA UJENZI AAHIDI SERIKALI KUKAMILISHA KUUNGA PIA MIKOA YA KATAVI, KIGOMA NA TABORA...

Barabara ya Tunduma-Ikana-Laela hadi Sumbawanga ikiwa imekamilika kwa asilimia mia moja (100%), barabara hii ambayo ni kiungo muhimu cha Mikoa ya Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma na Tabora imejegwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Msaada kutoka kwa watu wa Marekani.Waziri wa Wizara ya Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mjini Sumbawanga tarehe 02/02/2015 katika viwanja vya Nelson Mandela akiwa ziarani Mkoani Rukwa kukagua ujenzi unaoendelea wa barabara za lami za...

 

10 years ago

Bongo Movies

JB, Mzee Majuto na Richie Wamtembelea Mama wa Mtoto Albino Aliyeuawa…Wamwaga Machozi

Wikiendi iliyopita staa wa sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ alijikuta akiangua kilio na kuungwa mkono na mastaa wenzake, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ na Single Mtambalike ‘Richie’ walipomtembelea wodini mama mzazi wa mtoto Albino, Yohana Bahati (1) aliyeuawa kikatili, Ester Thomas (30) ambaye naye alijeruhiwa vibaya kichwani, Ijumaa Wikienda linakuhabarisha.

Tukio hilo la majonzi lilijiri kwenye Hospitali ya Bugando mkoani hapa ambapo wasanii hao walikwenda kumfariji mama wa mtoto huyo...

 

9 years ago

StarTV

Albino Aliyekatwa Mkono  kuruhusiwa hospitalini Lushoto

 

Hospitali ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga imesema wakati wowote itamruhusu mkazi wa kijiji cha Bungoi Ester Magamba baada ya afya yake kuimarika.

Ester ambaye ni mlemavu wa ngozi Albino alifikishwa katika hospitali hiyo baada ya watu kuvamia nyumbani kwake Desemba 8 na kumkata kidole chake cha mkono wa koshoto.

Tayari Jeshi la Polisi limemkamata mtu mmoja anayedaiwa kuhusika katika tukio hilo na linaendelea kuwatafuta watu wengine wawili..

Wilaya ya Lushoto, wilaya yenye sifa ya kilimo...

 

10 years ago

Uhuru Newspaper

Albino mwingine akatwa kiganja




Na Willy Sumia, Sumbawanga WAKATI Watanzania wakipaza sauti kukemea mauaji na ukataji viungo vya albino, mtoto mwingine Baraka Cosmas (6), amevamiwa na kukatwa kiganja cha mkono. Tukio hilo ambalo limezidisha hofu miongoni mwa albino nchini, limetokea usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Kipeta wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa. 
Habari za kuaminika zinasema kuwa, kundi la watu wasiojulikana walivamia kwenye nyumba aliyokuwa amelala Baraka na mama yake, Prisca Shaban na kuanza...

 

10 years ago

Habarileo

Albino mwingine akatwa kiganja

Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Jacob MwaruandaLICHA ya Serikali, jamii na jumuiya ya kimataifa kukemea ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), bado kuna wanaoendelea kung’ang’ania mila potofu za kuamini kwamba bila ya ushirikina unaohusishwa na matumizi ya viungo vya albino, hawawezi kufanikiwa kimaisha, iwe katika kisiasa au kibiashara.

 

10 years ago

Uhuru Newspaper

Polisi yawanasa 15 kiganja cha albino



NA WILLY SUMIA, SUMBAWANGAPOLISI mkoani Rukwa wanawashikilia watu 15, wakiwemo waganga wa kienyeji saba kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio la kukatwa kiganja cha mtoto Baraka Cosmas.Baraka (6), ambaye ni mlemavu wa ngozi, alikatawa kiganja cha mkono mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa amelala na mama yake usiku.Watuhumiwa hao walitiwa mbaroni kufuatia msako mkali unaoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani hapa, ikiwa ni muda mfupi baada ya tukio hilo.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa,...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani