Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Wanne wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua albino

>Washtakiwa wanne kati ya watano wa kesi ya kumuua mtu mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Henry Mwakajila mwaka 2008 wilayani Rungwe, wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa mjini hapa jana.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mwananchi

Wanne wahukumiwa kunyongwa kwa kuua albino Tanzania

Watu wanne wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na kosa la kumuua Zawadi Magindu (32) mwenye ulemavu wa ngozi, mkazi wa Kijiji cha Nyamaruru, Wilaya ya Geita mkoani hapa.

 

10 years ago

Vijimambo

WALIOMUUA ALBINO MWAKAJILA WA MBEYA LEO WAMEHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA

Hakimu Mwakalinga siku alipohukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Leo amehukumiwa tena kunyongwa mpaka kufa katika mauaji ya mlemavu wa ngozi Henry Mwakajila.

Na Daniel Mbega

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya leo hii imewahukumu kunyongwa mpaka kufa watu wanne kati ya watano waliomuua Henry Mwakajila (17) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino).


Waliohukumiwa kunyongwa mpaka kufa ni Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga na Gerard Korosso...

 

10 years ago

Habarileo

Ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua albino

MKAZI wa Kiwira, wilayani Rungwe, Hakimu Mwakalinga ambaye aliwahi kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kukutwa na hatia ya kumuua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Rungwe, John Mwakenja, amehukumiwa adhabu hiyo kwa mara nyingine baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mlemavu wa ngozi (albino).

 

10 years ago

Mtanzania

Walioua albino mwaka 2009 wahukumiwa kunyongwa

NA JUDITH NYANGE, MWANZA
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza imewahukumu kunyongwa washtakiwa watatu wa kesi ya mauaji ya Jesca Charles (25) mwenye albino, mkazi wa Igoma Kishiri wilayani Nyamagana, Mkoa wa Mwanza.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Agnes Bukuku baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili.
Washtakiwa hao ni Melikiadi Christopher (33) mkazi wa Igoma Kishiri, Yohana Kabadi (52) maarufu kama Mwanamalundi mkazi wa Igoma na Regina Mashauri (43) kutoka Mwisenya Igoma...

 

11 years ago

Mwananchi

Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga, imemhukumu Malambi Lukwaja (47) Mkazi wa Kijiji cha Igalula, Tarafa ya Kabungu, Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia.

 

10 years ago

Mwananchi

Mahakama yawahukumu watu Sita kunyongwa hadi kufa

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu kunyongwa hadi kufa  washtakiwa sita  katika kesi ya mauaji ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wa mkoani Morogoro na mfanyakazi wa Benki ya NMB.

 

10 years ago

CloudsFM

MTUHUMIWAWA MAUAJI YA MWANAFUNZI WA TEKU AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA.

ASKARImmoja kati ya watatu waliokuwa wakituhumiwa kwa mauaji kwa aliyekuwa mwanafunziwa Chuo kikuu TEKU, amehukumiwa kunyongwa hadi kufa huku wenzie wakiachiwahuru.

Hukumuhiyo ilitolewa katika Mahakama kuu kanda ya Mbeya na Jaji Rose Temba baada yakuridhishwa na ushahidi wa pande zote mbili uliotolewa mahakamani hapo kwanyakati tofauti.


Mwendeshamashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa akisaidiwa na Catherine Paul aliwatajawashtakiwa kuwa aliyehukumiwa ni Askari polisi F5842DC Maduhu na...

 

9 years ago

Dewji Blog

Mwanajeshi mstaafu Singida ahukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa

wooden gavel and books on wooden table,on brown background

Na Nathaniel Limu, Singida

MWANAJESHI mstaafu wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) mkazi wa kijiji cha Ighuka wilaya ya Ikungi mkoani Singida,Selemani Juma Karani (64),amehukumiwa na mahakama kuu kanda ya Dodoma adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

Karani amehukumiwa adhabu hiyo baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumpiga mshale wa sumu jirani yake Hadija Swalehe kichwani  upande wa kulia, na kutokezea sikio la kushoto na kusababisha kifo chake.

Mwendesha mashitaka wakili wa serikali...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani