Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


26 wakamatwa kwa uvamizi wa mashamba

Na John Gagarini, Kibaha
JUMLA ya watu 26 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kuharibu mazao ndani ya shamba.
Pia watu hao wanatuhumiwa kuvamia mashamba na kuingia kwa jinai kukutwa na bangi kete 38 na gramu 250 za bangi pamoja na pombe ya moshi lita 30.

Akithibitisha kwa kutokea tukio hilo alisema kuwa uvamizi huo ulifanywa kwenye vitongoji vitatu tofauti vya Mkonga, Mkombozi na Tambani wilayani Mkuranga.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

SABA WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI WA NOTI BANDIA ZA DOLA ZA KIMAREKANI WAKAMATWA

Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam akionesha noti bandia zilizokamatwaJeshi la Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata kundi la watu saba wanaotengeneza noti bandia za dola ya Kimarekani huko maeneo ya Sinza katika Hotel iitwayo Mombasa Kinondoni, jijini Dar es Salaam. 
Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 04/8/2014 wakiwa na noti bandia zipatazo 10,640 za dola mia (100) ambazo ni sawa na dola 1,064,000 ambazo ni zaidi ya shilingi za Kitanzania...

 

9 years ago

StarTV

Wachimbaji wadogo walia na Serikali kwa uvamizi maeneo ya machimbo

Wachimbaji Wadogo katika kijiji cha Samina wamedai kuwa Serikali haiwajali na imekuwa ikiwapa ahadi zisizokamilika hali iliyochangia wachimbaji hao kuvamia maeneo hatarishi na kujitafutia riziki.

Wakiongea na Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa wamesema kuwa waliahidiwa kutafutiwa maeneo ya uchimbaji lakini maeneo waliyopewa hayakuwa na dhahabu hali iliyokatisha tamaa na kuchangia kuongezeka kwa vijana wasio na ajira

Mkuu wa Mkoa Fatma Mwassa amewapa nafasi wachimbaji wataje maeneo...

 

9 years ago

StarTV

Watu wa nne wahukumiwa miaka 32 jela kwa uvamizi Nzega.

Mahakama  ya hakimu  mkazi wilaya ya nzega imewahukumu  kifungo cha miaka 32 jela watu nane kwa kosa la kufanya uvamizi na kuiba dhahabu tofali  sita na nusu zenye thamani ya zaidi ya hsilingi bilioni 4 katika mgodi wa dhahabu wa resolute

Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi silyvester  kainda amesema washitakiwa mawazo saliboko ,edward  bunera  ,shaaban  amuru,john  ndaki,pius  shija ,aloyce  zindoro ,davidi  ndaki  pamoja na frenk  kabuche wamehukumiwa  kwenda  jela miaka  30 baada  kutiwa...

 

11 years ago

Mwananchi

Mashamba ya Balali kugawanywa kwa wananchi

>Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero imeamua kufuta miliki ya mashamba yote makubwa yasiyoendelezwa na taratibu mpya zinafanyika ili kuyamilikisha kwa wananchi.

 

10 years ago

Michuzi

SHIWATA WAGAWA MASHAMBA KWA WANACHAMA WAKE

Msanii Maarufu nchini Ahmed Olotu 'Mzee Chilo' wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekita wa SHIWATA Cassim Taalib wa pili kushoto  walipokuwa wakigawa mashamba kwa ajili ya wanachama waoWatakaohamia kijiji cha wasanii kupewa bustani bure

Na Mwandishi Wetu

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umetoa bure kwa wanachama wake wanaomiliki nyumba katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga ya eneo la kulima bustani.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana...

 

11 years ago

Habarileo

Tanga wasitisha ugawaji wa mashamba kwa wageni

MKOA wa Tanga umesitisha ugawaji wa mashamba na maeneo ya malisho kwa wageni hadi utakapokamilisha upimaji ardhi yote na kuipangia matumizi.

 

9 years ago

Michuzi

EKARI 7000 ZA MASHAMBA KUGAIWA KWA WANANCHI WA ARUSHA.

SERIKALI imetwaa jumla ya Ekari 7000 baada ya ubatilishwaji wa Mashamba ya Tanzania plantatition limited yaliyokua yakimilikiwa na mwekezaji  kutoka nje ,mashamba hayo yanatajiwa kugawanywa kwa wananchi 2000 wenye uhitaji wa ardhi ya makazi na mashamba .
Aidha baada ya ubatilishwaji wa mashamba hayo Arusha imepata ekari 6176.5 na Halmashauri ya Meru ekari 925  hivyo kufikia ekari 7101 ambazo zitagawanywa kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi,Wiliam Lukuvi wakati...

 

10 years ago

Michuzi

TANGAZO LA VIWANJA NA MASHAMBA KWA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA (DIASPORA)

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaandaa mahitaji ya ardhi kwa ajili ya watanzania waishiao nje ya Tanzania.  Nchini Uingereza, Ubalozi unaratibu zoezi hilo kwa watanzania waishio Uingereza na Ireland. 
Tunaomba maombi hayo yaainishe Mkoa na Wilaya hitajika, aina ya matumizi ya ardhi hiyo kama ni Makazi, Biashara au Kilimo.
Maombi yawasilishwe kwa Viongozi wa Jumuiya za Watanzania katika miji/ maeneo wanayoishi, ambao watayaleta ubalozini kwa hatua zaidi. Au muombaji wanaweza...

 

9 years ago

StarTV

Wakazi Chekimaji wailaumu halmashauri ya Hai kwa Uharibifu wa Mashamba Ya Mpunga

Wakazi wa Kijiji cha Chekimaji wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wameulalamikia uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kushindwa kuwashirikisha katika ujenzi wa mradi wa Barabara yenye urefu wa kilomita 30 inayojengwa kwa kiwango cha Moramu kwa gharama ya shilingi bilioni 1.4.

Malalamiko hayo yanakuja kutokana na uharibifu mkubwa wa mashamba ya Mpunga baada ya ujenzi wa barabara hiyo inayopita katikati ya mashamba hayo kuanza mara moja.

Katika mkutano maalumu uliowakutanisha wakulima wenye...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani