Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Dewji Mtu wa Mwaka Afrika

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL), Mohammed Dewji maarufu Mo, ameshinda tuzo ya Mtu wa Mwaka barani Afrika wa jarida maarufu la Fobes (Forbes Africa Person Of the Year 2015), katika hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia jana jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

habarileo

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Bongo5

Forbes 2015: Dewji amtoa Rostam Aziz kwenye nafasi ya kwanza kama mtu tajiri zaidi Tanzania!

Mohammed Dewji ndiye mtu tajiri zaidi nchini Tanzania, kwa mujibu wa orodha ya mwaka 2015 ya mtandao wa Forbes wa mabilionea 32 barani Afrika. Awali ni Rostam Aziz ndiye aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo. Kwa mujibu wa Forbes, Dewji mwenye umri wa miaka 39 ana utajiri wa dola bilioni 1.3. Utajiri huo unamfanya mfanyabiashara huyo ambaye […]

 

10 years ago

Tanzania Daima

Mo Dewji azidi kunga’ra Afrika

MFANYABIASHARA maarufu hapa nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’, amezidi kung’ara katika biashara ambako safari hii amejumuishwa kwenye orodha ya mabilionea 55 wa Afrika. Mo ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mjini...

 

10 years ago

Vijimambo

Dewji sasa bilionea kijana Afrika

Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu nchini na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohammed Dewji (pichani) kwa mara ya kwanza ameingia kwenye orodha ya mabilionea 29, akiwa tajiri kijana kuliko wote barani Afrika.Jarida la Forbes la Marekani limemtaja Dewji (39), katika nafasi ya 24 ya matajiri wa Afrika akiwa na utajiri wa Dola 1.3 bilioni za Marekani (Sh2.34 trilioni) unaotokana na biashara mbalimbali anazozifanya kupitia kampuni yake ya Mohammed Enterprises (Metl Group). “Dewji alibadilisha...

 

11 years ago

Tanzania Daima

Dewji: Afrika tunaweza kutokomeza umaskini

MFANYABIASHARA maarufu hapa nchini, na Mbunge wa Singida Mjini,  Mohamed Dewji (CCM), amesema nchi za Afrika zina uwezo mkubwa wa kujikomboa katika lindi la umaskini iwapo sera nzuri zitatungwa na...

 

10 years ago

Habarileo

Dewji tajiri zaidi Afrika Mashariki

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mohammed `Mo’ Dewji (39), amezidi kupaa kwa utajiri, kiasi cha sasa kuwa ndiye bilionea kijana zaidi katika nchi za Afrika Mashariki, lakini pia akitajwa ndiye bilionea kijana zaidi barani Afrika.

 

9 years ago

Dewji Blog

Mo Dewji anyakua tuzo ya mwaka ya mfanyabiashara anayesaidia zaidi jamii

IMG_9463

 Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta Naicker akimkabidhi tuzo ya ‘2015 Philanthropist of the year-East Africa’ Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji katika sherehe zilizofanyika hoteli ya DusitD2 jijini Nairobi.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

IMG_9492

Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akizungumza kwenye hafla ya tuzo za All Africa Business Leaders Awards 2015 (AABLA). Kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta...

 

10 years ago

Mwananchi

FORBES: Dewji sasa bilionea kijana Afrika

>Mfanyabiashara maarufu nchini na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohammed Dewji (pichani) kwa mara ya kwanza ameingia kwenye orodha ya mabilionea 29, akiwa tajiri kijana kuliko wote barani Afrika.

 

10 years ago

Mwananchi

Dewji atunukiwa tuzo uongozi bora Afrika

Mbunge wa Singida Mjini (CCM) na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ameshinda tuzo ya kiongozi bora aliyejitolea kwa kiasi kikubwa katika jamii na kuleta mabadiliko Afrika kwa mwaka 2014.

 

9 years ago

Habarileo

Mo Dewji ang’ara tuzo wafanyabiashara Afrika

BILIONEA anayemiliki kampuni kubwa ya Mohammed Enterprises nchini (MeTL), Mohammed Dewji ‘Mo’ ameshinda Tuzo ya Mfanyabiashara wa Mwaka anayejitoa zaidi kuisaidia jamii kunufaika, kutokana na biashara zake, akiwa mshindi wa Afrika, Kanda ya nchi za Afrika Mashariki katika tuzo zilizofanyika juzi jijini Nairobi, Kenya.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani