Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Dude: Filamu Kwa Buku, ‘No’, Nasema Nooo!

Mwigizaji mkongwe wa filamu hapa nchini, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameiomba serikali iwasaidie kutokana na mpango uliowekwa wa kuuzwa filamu zao kwa shilingi elfu moja, jambo ambalo anaona litawafanya wasanii wazidi kuwa masikini.

Akizungumzia swala hilo, Dude alionesha kutokukubaliana na hatua hiyo na kueleza kuwa, endapo serikali italifumbia macho suala hilo, soko la filamu litakufa.

“Yaani nasema noooo, kiukweli filamu kuuzwa bei ya shilingi elfu moja wasanii tutakuwa hatuioni faida, ni bora...

Bongo Movies

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

GPL

DUDE: FILAMU KWA BUKU, ‘NO’, NASEMA NOOO!

Staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude. Stori: Shani Ramadhani
Staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameiomba serikali iwasaidie kutokana na mpango uliowekwa wa kuuzwa filamu zao kwa shilingi elfu moja, jambo ambalo anaona litawafanya wasanii wazidi kuwa masikini. Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Dude alionesha kutokukubaliana na hatua hiyo na kueleza kuwa, endapo serikali...

 

10 years ago

Bongo Movies

Dude akubaliana na bei ya Tshs. 1500 kwa filamu. Asema ndio njia pekee ya kupambana na uharamia.

Masanii wa filamu nchini Dude, amefunguka kwa kusema kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kupambana na wezi wa kazi za wasanii ni bora bei ya Steps Tsh 1500 iyendelee ili kuiyokoa tasinia hiyo.

Dude ameiambia tovuti ya Bongo5 kuwa hakuna njia kwa sasa ya kuweza kupambana na maharamia wa kazi za wasanii zaidi kushusha bei ya filamu.

“Tumeshindwa kuwathibiti pirates, watu wanasambaza kazi, wanauza kazi kwa bei rahisi, leo hii ukienda Buguruni unapata kazi kwa elfu mbili, elfu moja mia tano,...

 

10 years ago

GPL

MTITU ASHANGAA NISHA, JB KUKUBALI FILAMU ZA BUKU

Muongozaji, msanii na mmiliki wa Kampuni ya Filamu ya Five Effects, William Mtitu. Muongozaji, msanii na mmiliki wa Kampuni ya Filamu ya Five Effects, William Mtitu amewavaa wasanii wenzake wakiwemo Salma Jabu ‘Nisha’, Jacob Steven ‘JB’ na wengineo akidai wanatumiwa kuiua tasnia ya filamu Bongo kwa kukubali CD zao kuuzwa buku. Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Mtitu alisema Kampuni ya Steps imeamua...

 

10 years ago

Bongo5

Dude asema anakubaliana na Steps kuuza filamu moja Tsh 1,500

Masanii wa filamu nchini Dude, amefunguka kwa kusema kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kupambana na wezi wa kazi za wasanii ni bora bei ya Steps Tsh 1500 iyendelee ili kuiyokoa tasinia hiyo. Dude ameiambia leo Bongo5 kuwa hakuna njia kwa sasa ya kuweza kupambana na maharamia wa kazi za wasanii zaidi kushusha bei ya filamu. […]

 

10 years ago

Michuzi

Bodi ya Filamu Nchini yatoa wito kwa wamiliki wa Filamu kuweza kuwasilisha Filamu.

Lorietha Laurence -Maelezo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo  ametoa wito kwa kampuni za Filamu nchini kuwasilisha filamu zao ili ziweze kuhakikiwa na kulipiwa  kwa kupata kibali cha kuingia sokoni  kama sheria ya filamu ya mwaka 1976 kifungu namba 4 inavyoeleza.
Akizungumza  katika ofisi za Bodi leo jijini Dar es Salaam, Fisoo ameipongeza  kampuni ya Al-Riyamy Production  ambayo imeweza kutimiza wajibu wake na kulipia filamu 134 ambazo zimepata kibali cha kupatiwa stamp za  TRA...

 

10 years ago

Bongo5

New Video: Diamond atoa video mpya ‘Nasema Nawe’ kwa kushtukiza, kamshirikisha Khadija Kopa

Diamond Platnumz ameachia video mpya ya wimbo wake mpya uitwao ‘Nasema Nawe’ aliomshirikisha malkia wa Taarab Khadija Kopa kwa kushtukiza. Tumezoea kuona video nyingi za miaka ya karibuni za Diamond zimekuwa zikifanyika nje na madirector wa nje, lakini video hii imeongozwa na director mpya wa Tanzania Hanscana na imefanyika hapa hapa nyumbani.

 

10 years ago

Bongo Movies

Sakata la kushushwa kwa bei za filamu.Watayarishaji filamu nao waibuka

Bodi ya Filamu kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara, TRA, TBS, imekuwa ikifanya vikao vya ndani zaidi ya viwili sasa na wasambazaji wa filamu ili kuzungumzia suala ya bei ya filamu. “Tunaiomba serikali kupitia vyombo vyake vyote vinavyoshiriki haya masuala ya filamu, kusifanyike mkutano wa aina yoyote ile kuzungumzia bei ya filamu bila kushirikisha maprodyuza, sisi ndiyo wenye filamu na ndiyo tunaotengeneza sasa...

 

9 years ago

Bongo5

Picha: Muongozaji wa filamu wa Tanzania ashinda tuzo za Marekani na kuwashangaza kwa ubora wa filamu zake

Pamoja na wengi kuamini kuwa ubora wa filamu za Tanzania ni mdogo, wapo vijana wanaofanya filamu tofauti zinazowashangaza hadi wataalam wa industry hiyo nchini Marekani. Timoth Conrad akiwa na tuzo aliyoshinda hivi karibuni nchini Marekani Mmoja wa vijana hao ni Timoth Conrad Kachumia ambaye mwezi huu alishinda tuzo kwenye tamasha la Silicon Valley African Film […]

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani