Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Jenerali Mwamunyange awafunda wakufunzi

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Devis Mwamunyange amesema katika kuendeleza juhudi za Serikali juu ya kuboresha mafunzo ya JKT nchini, wakufunzi wa mafunzo hayo wanapaswa kufuata maadili ya taaluma yao katika utekelezaji wa majukumu waliyokabidhiwa na jeshi hilo.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Vijimambo

Jenerali Mwamunyange sasa aibukia Ngerengere.

\Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, (pichani) ameibukia katika Kamandi ya Anga Kizuka iliyopo Ngerengere, mkoani Morogoro wakati Rais Jakaya Kikwete, akizindua uwanja wa Ndege wa Kamandi hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Rais Kikwete alisema kuwa katika miaka 10 ya uongozi wake, amefanya mambo mengi kwa Watanzania pamoja na kuliacha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likiwa katika hali nzuri ya kiutendaji.
Alisema hakuna nchi inayoweza kupata maendeleo...

 

9 years ago

Habarileo

‘Waliomzushia Jenerali Davis Mwamunyange waombe radhi’

WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, imewataka watu waliosambaza uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, kuwa amelazwa nje ya nchi kwa ugonjwa, kuomba radhi mapema la sivyo watachukuliwa hatua.

 

9 years ago

Mtanzania

Mahakama yakusudia kumpa dhamana aliyemzushia Jenerali Mwamunyange

Davis MwamunyangeNA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, inaangalia mwelekeo wa kumpa dhamana mwanafunzi wa Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT), Benedict Ngonyani, anayetuhumiwa kusambaza taarifa za uzushi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, amelishwa sumu.

Hayo yalidaiwa jana mahakamani hapo, wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa na upande wa Jamhuri na kudai kuwa upelelezi haujakamilika.

Hakimu Mkazi Respicius Mwijage, aliahirisha kesi hiyo...

 

10 years ago

Vijimambo

MAMLAKA ZA MISHENI ZA ULINZI WA AMANI ZIWE WAZI-JENERALI MWAMUNYANGE

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akiwa katika ukumbi wa Baraza la Uchumi la Umoja wa Mataifa maarufu kama ECOSOC ambapo ndipo ulipofanyika mkutano wa kihistoria wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Maafisa wa ngazi za juu kutoka nchi zinazochangia katika Operesheni za Ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa. Akichangia majadiliano ya mkutano huo. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi amelishauri Baraza Kuu la Usalama na UN kuweka bayana na kwa uwazi mamlaka ya misheni ...

 

9 years ago

Mwananchi

Brigedia Jenerali Njau awafunda wahitimu JKT

Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Kamandi ya Nchi Kavu, Brigedia Jenerali Francis Njau amesema lengo la Serikali kutoa mafunzo ya kujitolea kwa vijana nchini ni kutaka kuwawezesha kujiajiri.

 

11 years ago

Michuzi

mkuu wa majeshi jenerali Davis Mwamunyange na ujumbe wake wakiwa Dubai

 Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na ujumbe wake, akiwa na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga, wakiwa katika picha ya pamoja na mtumishi wa Hoteli ya Continental ya Dubai, ambaye kwa sasa ndiye Mtu Mrefu Duniani.

 

9 years ago

Mtanzania

Kaka wa Jenerali Mwamunyange naye akanusha mdogo wake kulishwa sumu

Davis MwamunyangeNa Victoria Patrick, Dar es Salaam

KAMISHINA Msadizi na Mwandamizi  mstaafu wa Jeshi la Polisi, Aden Mwamunyange ambaye ni kaka wa Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange, naye amekanusha taarifa   zilizoenezwa hivi karibuni katika mitandao ya  jamii kuwa amelishwa simu.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Jeti Lumo,  Dar es Salaam jana, alisema hizo taarifa hizo si za kweli na ni uzushi.

“Mimi kama mwana familia nakanusha taarifa hizo...

 

10 years ago

Michuzi

MAMLAKA ZINAZOHUSU OPERESHENI ZA ULINZI WA AMANI ZIWE WAZI- JENERALI MWAMUNYANGE

Na Mwandishi Maalum, New York Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, amelishauri Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuweka bayana na kwa uwazi mamlaka ( mandate) ambayo misheni ya kulinda Amani itapaswa kutelekeza kule inakopangiwa kwenda.  Ametoa ushauri huu siku ya Alhamisi wakati alipokuwa akitoa mchango wake kwenye mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi ambao nchi zao zinachangia katika operesheni za ulinzi wa Amani za...

 

10 years ago

Michuzi

MKUU WA MAJESHI TANZANIA JENERALI DAVIS MWAMUNYANGE AFUNGUA KIWANJA KIPYA CHA MICHEZO

 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange  akifungua kiwanja kipya cha Michezo kitakachotumika kwa ajili ya michezo ya Majeshi ya Shirikisho la Jumuia ya Afrika Mashariki, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi na kushoto ni Mkuu wa Brigedi ya Nyuki, Brigedia Jenerali Sharif  Sheikh Othman. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange akimpongeza Mkandarasi wa kiwanja hicho kutoka Kampuni ya M. S Maya Heardwere ya Zanzibar Bw. Abdallah...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani