Magufuli ashusha rungu Muhimbili
RAIS Dk John Magufuli ameanza kudhihirisha kuwa serikali yake haitakuwa na simile kwa watendaji wazembe baada ya jana kuivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) pamoja na kumuondoa madarakani Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Dk Hussein Kidanto.
habarileo
Habari Zinazoendana
11 years ago
Uhuru Newspaper02 Jul
Mufti Simba ashusha rungu, ang’oa uongozi
NA SHAABAN MDOE, ARUSHA
SHEIKH Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bn Simba, ametangaza kuung’oa uongozi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa na ule wa Quba jijini Arusha na kutangaza uongozi mpya.
Amesema uongozi huo, utakaa madarakani hadi pale atakapofanya mabadiliko mengine ikilazimika.
Kutangazwa kwa uongozi huo, kumetengua kitendaliwa cha muda mrefu kuhusu viongozi halali wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) kwa wilaya ya Arusha na mkoa wa Arusha.
Kabla ya kutangaza uamuzi huo, Mufti...
9 years ago
Mwananchi09 Oct
Dk Magufuli ashusha neema ya barabara Moshi
9 years ago
Habarileo01 Dec
Magufuli ashusha maelekezo mashirika ya umma
RAIS John Magufuli ametoa maelekezo ya utendaji uliotukuka kwa wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma na watendaji ili kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa bora na kuepuka matumizi ya ziada yasiyokuwa ya lazima.
9 years ago
Habarileo07 Sep
Dk Magufuli afunika Moro, ashusha neema
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli, amesema Serikali atakayoiongoza itajenga viwanda vikubwa, vya kati na vidogo ili kuongeza ajira na mapato ya Serikali, huku akiwaahidi wakazi wa Morogoro kufufua viwanda vyao.
9 years ago
Mtanzania01 Dec
Rungu jipya la Magufuli
*Fagio la kupunguza wafanyakazi mashirika ya umma
*Posho za wabunge vikao vya bodi zapigwa marufuku
RUTH MNKENI NA JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM
SERIKALI ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli, imeshusha rungu jipya kwa kutangaza uamuzi mchungu wa kupunguza wafanyakazi katika taasisi na mashirika ya umma ambayo yameonekana kuwa mzigo katika utendaji.
Mashirika hayo yameelezwa licha ya kuwa na watumishi wengi, lakini bado uzalishaji na utendaji wake umekuwa hauna tija kwa taifa.
Hayo...
9 years ago
Mtanzania30 Nov
Rungu la Magufuli latua kwa Bakhresa
*TRA yazuia makontena yake bandari kavu
*Polisi yasema uchunguzi mzito unaendelea
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imezuia kampuni ya Said Salim Bakhresa & Co. Limited kupeleka makontena yake katika Bandari yake Kavu (ICD), baada ya kugundulika kuwa baadhi ya makontena yalipitishwa bila kulipiwa kodi.
Kwa mujibu wa barua ya TRA ya Novemba 17, mwaka huu, iliyosainiwa na Wolfagang Salia kwa niaba ya Kamishina wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, kampuni hiyo...
9 years ago
Mtanzania12 Nov
TRA: Rais Magufuli ametupa rungu
NA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema kuanzia sasa inaanza kutekeleza agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuwakamata wafanyabiashara watakaokwepa kulipa kodi na kuwafikisha mbele ya vyombo vya dola.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade, alisema uamuzi wa kuwakamata wafanyabiashara ambao siku za nyuma walikuwa wakikingiwa kifua na watendaji wa Serikali, utaanza mara moja baada ya kupata baraka za Rais...
9 years ago
Mtanzania23 Nov
Magufuli aitikisa Muhimbili
*Uongozi wahaha siku za mapumziko
* Sefue leo kufanya ukaguzi, kufuatilia maagizo
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UAMUZI wa Rais Dk. John Magufuli kumng’oa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Hussein Kidanto, umesababisha wafanyakazi wa hospitali hiyo na viongozi wao kufanya kazi hadi siku za mapumziko.
Hatua hiyo imekuja wiki chache baada ya Dk. Magufuli, kufanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Novemba 9 ikiwa ni ziara yake ya pili baada ya ile...
9 years ago
Mtanzania10 Nov
Magufuli aifumua Muhimbili
*Amng’oa mkurugenzi mkuu, avunja bodi
*Asononeshwa wagonjwa kulala chini
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
RAIS John Magufuli, amemng’oa Kaimu Mkurugenzi wa Hopitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Hussen Kindato pamoja na kuvunja bodi ya wakurugenzi wa hospitali hiyo.
Hatua hiyo ameichukua jana baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo, ambapo alipofika alikagua maeneo yote, kutembelea wodi na kushuhudia idadi kubwa ya wagonjwa wakiwa wamelala chini kwa kukosa vitanda.
Taarifa...