Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


mpiganaji Edson Kamukara afariki dunia


Mhariri  wa Mwana Halisi Online, Edson Kamukara (pichani), amefariki Dunia kwa ajali ya moto nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam leo hii majira ya saa moja kasorobo jioni, baada ya kulipukiwa na jiko la gesi, habari zilizotufikia sasa hivi zinasema kuwa Polisi wameuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuhifadhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa kifo chake.


Ofisa Uhusiano wa NMB, Viccent Mnyanyika akimkabidhi zawadi marehemu Edson Kamukara wakati wa uhai wake...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Vijimambo

VIONGOZI WA CHADEMA WALIVYOSHIRIKI MAZISHI YA MWANAHABARI EDSON KAMUKARA

Jeneza lililobeba mwili wa mwanahabari Edson Kamukara likiwa limewekwa tayari kwa kutoa heshima za mwisho na kwenda kuzikwaMwenyekiti wa CHAHDEMA Mh Freeman Mbowe akitoa salamu za mwisho kwa mwili wa marehemu Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club.Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa akitoa salamu za mwisho wakati wa kuaga mwili wa marehemu Edson Kamukara.Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akisalimiana na Mkurugenzi wa Hali Halisi Ndugu Said Kubenea wakati wa kuaga mwili wa...

 

10 years ago

Dewji Blog

Salamu za rambirambi kutoka TGNP kufuatia kifo cha Edson Kamukara

Mwana Halisi Online, Edson Kamukara

Marehemu Edson Kamukara enzi za uhai wake.

Salamu Za Rambirambi Kutoka TGNP- Kifo Cha Kamukara 

 

10 years ago

Vijimambo

ALIYEKUWA MHARIRI WA KAMPUNI YA MWANAHALISI, EDSON KAMUKARA KIJIJINI AZIKWA BUKOBA


Na Faustine Ruta, Bukoba.Mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Salvatory Kamukara aliyefariki alhamisi ya wiki iliyopita jijini Dar es Salaam umezikwa leo Nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera katika Kijiji cha Ihangiro kitongoji cha Bukujungu na kuagwa na mamia ya waombolezaji.Marehemu Edson alizaliwa 27,03.1980 na kufariki wiki iliyopita juni 25, 2015 na amezikwa jana Jumatatu juni 29, 2015. Marehemu walizaliwa Mapacha na ameacha Pacha mwenzake Edda na  ameacha Mtoto...

 

11 years ago

Michuzi

MPIGANAJI MAXIMILIAN NGUBE AFARIKI DUNIA

MPIGA PICHA MKONGWE WA PICHA ZA TELEVISHENI,MAXIMILIAN NGUBE (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA LEO ASUBUHI BAADA YA KUSUMBULIWA KWA MARADHI KWA MUDA MREFU.
MAREHEMU MAXIMILIAN AMBAYE ALIFAHAMIKA SANA KWA JINA LA PAPAA MAX,ALIKUWA NI MPIGA PICHA HODARI WA KITUO CHA TELEVISHENI CHA MLIMANI TV.
GLOBU YA JAMII IMEPOKEA TAARIFA ZA MSIBA HUU KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA NA TUNAMUOMBEA KWA MWENYEZIMUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAXIMILIAN NGUBE MAHALI PEMA PEPONI.
-AMIN.

 

10 years ago

Michuzi

Mpiganaji Kyaloeichi Oko Kessy afariki dunia

Mwandishi mkongwe wa habari, Kyaloeichi Oko Kessy (62) amefariki dunia usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Pugu jijini Dar es Salaam.
Mpwa wa marehemu Tumaini Msengi amesema hayo leo kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu kwa muda mrefu na amekuwa akitibiwa katika hospitali mbalimbali za jijini Dar es Salaam hadi jana ambapo mauti yalimkuta.
Kabla hajaanza kuugua Kessy alikuwa mwandishi wa kujitegemea akiandika zaidi uchambuzi na makala katika vyombo...

 

10 years ago

Dewji Blog

Mamia wajitokeza viwanja vya Leaders Club Jijini Dar kumuaga Mhariri Edson Kamukara

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Kamukara wakati ulipowasili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam jana asubuhi, kwa ajili ya kuagwa. Kamukara alifariki dunia juzi na mazishi yake yanatarajia kufanyika nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Reginald Mengi (katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilibrod Slaa kwenye...

 

10 years ago

GPL

MAMIA WAJITOKEZA VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR ES SALAAM KUMUAGA MHARIRI EDSON KAMUKARA

 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Kamukara wakati ulipowasili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo asubuhi, kwa ajili ya kuagwa. Kamukara alifariki dunia juzi na mazishi yake yanatarajia kufanyika nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera.…

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani