Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Makamba: Waliochota Escrow wabanwe zaidi

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema watu wote waliohusika katika sakata la kuchukua Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow wachukuliwe hatua kali za kinidhamu na kisheria ili iwe fundisho kwa viongozi wengine wenye kutumia madaraka yao vibaya.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mtanzania

Saa za waliochota Sh bil 321 IPTL zahesabika

Abdulrahman Kinana

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kila aliyehusika katika kashfa ya uchotwaji wa Sh bilioni 321 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), abebe msalaba wake bila kujali cheo chake na kwamba muda wa kulindana umekwisha.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye walipokuwa wakihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Ilulu...

 

10 years ago

Mtanzania

Zitto: Escrow ni zaidi ya Muhongo

Zitto_Kabwe_2011Fredy Azzah na Nora Damian, Dar es Salaam
SIKU moja baada ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kutangaza kujiuzulu kutokana na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema suala hilo bado ni bichi.
Pamoja na hali hiyo, PAC imesema hadi sasa Serikali imetekeleza maazimio manane ya Bunge kwa asilimia 35.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za...

 

10 years ago

Habarileo

Ataka siku zaidi mjadala wa Escrow

Livingstone LusindeMBUNGE wa Mtera, Livingston Lusinde (CCM), ametaka kutengwa siku zaidi ya moja za kujadili ripoti ya sakata la akaunti ya Tegeta Escrow bungeni.

 

10 years ago

Mwananchi

Zitto: Yanayoendelea biashara ya sukari ni zaidi ya escrow

Baada ya Watanzania kuliona Bunge likiwachukulia hatua vigogo waliohusika na ufisadi wa Akaunti ya Tegeta Escrow wa Sh306 bilioni, madudu mengine ya Serikali yanatarajiwa kubainika mara bada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuanza kufuatilia sakata ya sukari nchini. Hatua hiyo ya PAC kuanza kulifanyia kazi inatokana na malalamiko ya wamiliki wa viwanda vya sukari yanayotolewa kutokana na soko la ndani kutekwa na sukari inayoingizwa kutoka nje ya nchi na wafanyabiashara...

 

10 years ago

StarTV

Hatua zaidi zatakiwa kuchukuliwa wahusika wa ESCROW.

Na Blaya Moses,

Dodoma.

 

Wakati baadhi ya wananchi na taasisi mbalimbali nchini zikiendelea kushinikiza uwajibishwaji wa baadhi ya viongozi waliohusika na wizi kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, umoja wa shirikisho la chuo kikuu cha Dodoma umeshauri hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya wahusika wote kwani kuvuliwa nyadhifa zao pekee haitoshi.

Aidha shirikisho hilo limempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuanza kuwawajibisha baadhi yao likimshauri kuendelea pia kuwashughulikia wale wote...

 

10 years ago

Mwananchi

Ni gharika kwa watu zaidi ya 50 sakata la Escrow

>Moto wa kashfa ya ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow unaoendelea kuwaka bungeni, sasa unaonekana kugeuka gharika inayoweza kuwakumba vigogo wengi zaidi na kuiweka Serikali ya Rais Jakaya Kikwete katika hali ngumu.

 

11 years ago

Tanzania Daima

‘Wabunge wabinafsi wabanwe’

WANANCHI wamelitaka Bunge kuunda sheria zitakazowafanya wabunge kuwajibika ipasavyo katika shughuli za Bunge na umma kwa ujumla kwa kuweka pembeni  maslahi binafsi. Wakizungumza na Tanzania Daima jana kuhusu tuhuma za...

 

10 years ago

Mwananchi

‘Wachafuzi mitandaoni wabanwe’

Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kutoka vyuo vikuu, wamekitaka chama hicho kuchukua hatua za makusudi kutokana na kuanza kushamiri kwa taarifa za watu kuchafuana kupitia mitandao ya kijamii.

 

11 years ago

Habarileo

JK aagiza madereva wabanwe

RAIS Jakaya Kikwete ametaka vyombo vya ulinzi na usalama kutolegeza kamba katika kuchukua hatua dhidi ya madereva wasio makini na wazembe.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani