Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Twiga Stars yafuzu michezo Afrika

MSHAMU NGOJWIKE NA FARAJA MASINDE, DAR ES SALAAM
TIMU ya soka ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’, jana ilifuzu kwa mbinde fainali za Michezo ya Afrika ‘All African Games’ baada ya kuchapwa mabao 3-2 na Zambia ‘Shepolopolo’.
Licha ya kipigo hicho, Twiga Stars imenufaika na ushindi wa mabao 4-2 iliyoupata kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Lusaka, Zambia na hivyo kufuzu kwa jumla ya mabao 6-5.
Fainali za michuano hiyo zimepangwa kufanyika Congo, Brazzaville...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mwananchi

Twiga Stars yafuzu kwa kipigo

Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ imefuzu kushiriki Michezo ya Afrika mwezi Septemba nchini Congo-Brazaville licha ya kufungwa na Zambia (She-polopolo) kwa mabao 3-2 katika mchezo mkali uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 

10 years ago

GPL

Twiga Stars yapigwa, yafuzu All Africa Games

Wachezaji wa Twiga Stars wakishangilia goli.
Na Ibrahim Mussa, Dar es Salaam
TWIGA Stars imefuzu kushiriki Michezo ya Afrika ‘All African Games’ itakayofanyika Congo Brazzaville, Septemba mwaka huu, licha ya kufungwa mabao 3-2 na Zambia ‘Shepolopolo’ jana Ijumaa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hiyo imefuzu kwa jumla ya mabao 6-5, kwani katika mchezo wa awali nchini Zambia, Twiga ilishinda...

 

10 years ago

Mwananchi

Serikali sasa kutoa hatima ya Twiga Stars kucheza Afrika

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imesema Aprili 11 itaweka wazi hatma ya timu ya soka ya wanawake (Twiga Stars) kushiriki au la michezo ya Afrika ya Septemba nchini Congo Brazzaville.

 

9 years ago

Dewji Blog

Timu ya Taifa ya wanawake Twiga stars ‘Kimeeleweka’ wapaa Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African Games)

unnamed (78)Wachezaji wa Timu ya Taifa wakipanda ndege ya Shirikia la Ndege la Tanzania (Air
Tanzania) jana jioni  tayari kwa kuanza
safari ya kuelekea nchini Congo Brazaville kwa ajili ya Mashindano ya Afrika
(All African Games).

unnamed (77) Afisa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Gordon Nsajigwa akimpatia mmoja wa wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake tiketi  jana jioni tayari kwa safari ya kuelekea Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African Games),...

 

9 years ago

Michuzi

Timu ya Taifa ya wanawake Twiga stars yaondoka kuelekea Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African Games)

 Afisa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Gordon Nsajigwa akimpatia mmoja wa wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake tiketi  jana jioni tayari kwa safari ya kuelekea Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African Games), kushoto aliyevaa suti ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo.  Wachezaji wa Timu ya Taifa wakipanda ndege ya Shirikia la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) jana jioni  tayari kwa kuanza safari ya...

 

9 years ago

Michuzi

STARS YAFUZU HATUA YA PILI

TANZANIA imetimiza ndoto za kutinga hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia, licha ya kufungwa 1-0 na Malawi jioni ya leo katika Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre.

Tanzania inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1, baada ya Jumatano kushinda 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa hatua ya kwanza ya mchujo.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa wa Angola, Martins de Carlvalho aliyesaidiwa na Gadzikwa...

 

10 years ago

BBCSwahili

Afrika Mashariki yafuzu wavu ya ufukweni

Rwanda ndio mabingwa wa michuano ya mpira wa wavu wa ufukweni kwa wanawake yaliyofanyika katika Pwani ya Mombasa, nchini Kenya.

 

9 years ago

Mwananchi

Twiga Stars kibaruani

Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake, Twiga Stars inalazimika kucheza kufa na kupona leo ili kuhakikisha inapata ushindi dhidi ya Nigeria na kufufua matumaini ya kusonga mbele katika mashindano ya Afrika yanayoendelea Congo Brazzaville.

 

11 years ago

Mwananchi

Twiga Stars yatolewa

Ndoto ya Tanzania kucheza fainali za Afrika za wanawake mwaka huu zimefutika baada ya Twiga Stars kulazimishwa sare 1-1 na Zambia na hivyo kuondolewa kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2 jana kwenye Uwanja Azam Complex.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani