Warioba: Msichague wasiojua historia
WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amehadharisha umma wa Watanzania kuepuka kumkubali na kumchagua kiongozi asiyejua historia ya nchi, ilikotoka na ilipo. Akieleza kushangazwa na kile alichokiita ‘wimbo’ kwamba CCM haijafanya chochote katika miaka 54 tangu ipate huru, aliwashangaa zaidi watu wanaotumia jina la Mwalimu Julius Nyerere, mwasisi wa taifa, huku wakimuona dira, lakini wakisisitiza kwamba, hakufanya chochote.
habarileo
Habari Zinazoendana
11 years ago
Habarileo07 Feb
Nape: Kiborloni msichague wapinzani
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ametaka wananchi wa Kata ya Kiborloni mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kutochagua chama cha upinzani. Nape alisema hayo jana wakati akimnadi mgombea udiwani wa CCM, Kata ya Kiborloni, Willy Aidando kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika katika viwanja vya Shah Tours katika Manispaa ya Moshi.
11 years ago
Habarileo25 Mar
Nape: Chalinze msichague wapinzani
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ameasa wananchi Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kutofanya majaribio katika kupiga kura. Amewataka kuepuka kuchagua vyama vya upinzani, akisema vinatumia muda mwingi kufanya maandamano na migomo, badala ya kutatua kero za wananchi.
11 years ago
Dewji Blog06 Oct
Watanzania msichague Mafisadi — Kasesela
Na Mwandishi wetu
WATANZANIA wametakiwa kuwaadabisha kwa kutowachagua viongozi mafisadi wanaotaka kuingia madarakani kwa kutumia fedha chafu, katika chaguzi zijazo.
Kauli hiyo, ilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Madini nchini, Richard Kasesela (pichani) wakati wa ibada ya kuiombea nchi amani na mafanikio ya ujenzi wa Chuo cha Biblia mkoani Mbeya, yalifanyika katika Kanisa la Hossana Life Mission jijini Dar es Salaam.
Alisema endapo mafisadi hao wataingia madarakani katika cha guzi za...
11 years ago
Habarileo27 Sep
Kinana: Msichague viongozi wezi
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ametaka wananchi kutochagua viongozi wenye tabia ya wizi na dhuluma.
10 years ago
Habarileo12 Apr
Msichague wanaopenda matukio, Watanzania waaswa
WATANZANIA wametakiwa kuepuka kuwachagua viongozi wanaopendelea matukio kuliko kujali wananchi wao.
10 years ago
Mwananchi18 Jan
Kiswahili ni cha wasiojua Kiingereza?
10 years ago
Habarileo30 Aug
Askofu: Msichague wagombea wenye makandokando mengi
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk Barnabas Mtokambali, amewataka Watanzania kumkataa mgombea mwenye makandokando ya ufisadi na rushwa na kuelekeza nguvu kwenye masanduku ya kura ili wezi na mafisadi wasipate uongozi.
11 years ago
Mwananchi11 Feb
Ripoti:Wasiojua kusoma na kuandika waongezeka
11 years ago
Habarileo05 Feb
Wasiojua kuandika wasomea gesi Veta
WANAFUNZI 64 waliojiunga katika Chuo cha Mamlaka Ufundi Stadi (Veta) mjini Lindi mkoani humo mwaka jana, baadhi yao wamebainika hawajui kusoma wala kuandika.